Header Ads

header ad

WANANCHI WAMETAKIWA KUTUMIA TAKA KAMA NJIA YA KUINGIZA KIPATO




Wananchi  wametakiwa kubadilika na kutumia taka kama njia ya kujiingia kipato kufanya hivyo kutawaletea faida kwao, kwani takataka zikiwekwa kwa mpangilio Mzuri  huweza kuuzwa na kuwawezesha wao kupata kipato cha kujikimu .

Akizyngumza na SalvaNews Mkurugenzi wa Kampuni ya Kajenjere ambao  ni huhusika na kukusanya taka katika eneo la kata ya Mchikichini, Ilala, amesema Taka ni mali na masoko yapo waziwazi hakuna sababu ya mwananchi kutupa taka, wananchi wanatakiwa wajue kuwa taka ni pesa na wao kama (Kajenjere Trading Company) wamekuwa wakitoa  elimu ili wanaanchi wajue jinsi wanavyoweza kupata pesa.

Kutokana na wananchi kutokuwa na uelewa juu ya namna ya kuhidhi takataka ili baadae ziweze kuwaletea kipato Ammada Abubakari  ni bwana afya kutoka kampuni hiyo amesema taka zinaweza kutengeneza bidhaa mbalimbali na soko lake liko hapa hapa nchini ila tu wananchi wanapaswa kuzitenganisha kwa kila taka kukaa sehemu yake na kwa sisi tukienda na gari tunapa laki mbili mpka laki mbili na nusu kwa gari moja
Kwa hiyo wananchi wanapaswa kulitambua hilo
Kwa upande wao baadhi ya wananchi wa jiji la Dar es salaam wameonesha kutokuwa na uelewa juu ya faida za takataka na kuiomba serikali kuongeza elimu kwao  ili iweze kufika nchi nzima.

Naye  Afisa Mahusiano wa halimashauri ya manispaa ya ilala Tabu shaibu amesema wamekuwa na utaratibu mbali mbali za  kuwaelimisha jamii juu ya kutenganisha takataka huku wakiwekeza kwa wanafunzi wa shule.

Maarifa ya nchi mbalimbali yanaonyesha kuwa kugawanya aina tofauti za takataka kunasaidia mzunguko wa rasiliamali na kutatua tatzo la uchafu wa takataka mijini kwa mfano mji wa new York nchini  Marekani ni mji wa kisasa na kuvutia lakini mwaka  1895 mhandisi George Waring alianzisha mfumo wa kwanza wa kugawanya aina tofauti za takataka ili kuzitumia tena mjini humo hali iyosaidia.


Mkurugenzi wa Kampuni ya Kajenjere  Martine Andrew, akitoanuzi kwa mwandishi wa SalvaNews ofisi kwake kariakoo alipotembelewa mapema wiki hii.


Wafanya Usafi wa kampuni ya kajenjere wakiendelea na Usafi maeneo ya karume jijini dar es salaam.




Wakusanya taka  wakiendelea na kazi yao










Namna ambayo takataka zinatakiwa kuhifadhiwa





Na James Bayachamo-Salvanews

No comments

Powered by Blogger.