HISTORIA UJERUMANI YATWAA UBINGWA WA MABARA
Timu ya taifa ya Ujerumani imetwaa taji la kombe la mabara baada ya kuishinda Chile kwa bao 1-0 katika mchezo uliochezwa kwenye dimba la Saint Petersburg nchini Urusi.
Mshambuliaji Lars Stindl ndie aliyeifungia Ujerumani goli pekee liliwapa ubingwa wa mabara kwa mara ya kwanza baada ya kutumia vyema makosa ya kiungo wa Chile, Marcelo Diaz.
Katika mchezo wa kumsaka mshindi wa tatu Ureno walifanikiwa kutwaa medali ya shaba baada ya kuichapa Mexico kwa mabao 2-1.
Beki wa Ureno Luis Neto aliwapa Mexico goli la kuongoza baada ya kujifunga katika dakika ya 55, kabla ya Pepe kuzawazisha goli hilo katika dakika za lala salama.
Bao la mkwaju wa penati lilifungwa na Adrien Silva katika dakika ya 104 likawapa Ureno ushindi muhimu licha ya kumkosa nyota wake Cristiano Ronaldo.
Post a Comment