SINGIDA UNITED YANUNUA BASI LENYE THAMANI YA MILIONI 350
Club ya Singida United Leo imetambulisha basi lake jipya kwa wanahabari lenye thamani ya million 350 kwa ajiri ya wachezaji wa timu hiyo iliyopanda daraja kucheza ligi kuu kwa msimu wa 2017/2018.
Akizungumza na wandishi wa habari jijini Dar es salaam mwenyekiti wa kamatia ya usajili wa singida utd Festo Sanga amesema Kuwa club hiyo inaendeshwa kwa mfumo wa kampuni na uongozi umeona ni bora wajitegemee kwenye upande wa usafiri na Basi limenunuliwa kwa pesa za clabu na linamilikiwa na singida utd na club inajivunia kwa hilo Maana ni hatua kubwa kwao Maana timu nyingine zimeshidwa kufika hatua hiyo.
Aidha amesema kuwa club hiyo inaanza kambi kesho huko mkoa mwanza na wanategemea Leo watasafiri kwenda mwanza, na mpka sasa wanawachezaji 23 ikiwa ni 11 waliopanda na timu huku 6 wakiwa ni wa kimataifa waliowasajiri huku wa nne wakiwa wamewasajiri wa hapa nchini.
Sanga Amesema kuwa kwa sasa uwanja wao wa nafua wa huko mkoa singida unaendelea kujengwa mpka sasa uko kwenye hatua vizuri na wahusika wa ujenzi wa kiwanja hicho ni wabunge wa chama cha mapinduzi (ccm),wa mkoa huo na kusimamiwa na mkurugenzi wa mkoa na mwenyekiti wa chama cha ccm mama mrata na kudai kuwa mechi za kwanza za nyumbani wataanza kuchezea hapo
Katika hatua nyingine amekanusha madai ya baadhi ya mshabiki wanaodai kuwa singida utd ina uyanga na usimba jambo ambao halina ukwel na wao ni timu inayojitegemea na imejipanga kwa ligi na kupambana na timu yoyote ya ile ya ligi kuu msimu ujao.
Mpaka sasa club hiyo yanye maskani yake mkoani Singida ina wadhamini mbali mbali wakiwemo SportPesa,Oryx energy ,Halotel,Nmb na puma energy.
Basi aina ya dragoni ambalo singida utd wamelinunua kwa shilingi millioni 350.
Na James Bayachamo-Salvanews
Post a Comment