BANK OF AFRICA YAWAKARIBISHA WANANCHI KATIKA BANDA LAO ILI KUPATA HUDUMA MBALIMBALI KATIKA MAONYESHO YA SABASABA
Afisa Mahusiano wa BANK OF AFRICA tawi la Tandika Bi. Beatrice Richard akimkabidhi zawadi ya (Tyre Cover) Bw. Kevin Kihega kutoka mkoani Iringa aliyetembelea banda la benki hiyo lililopo Namba 85 Sabasaba Hall katika maonyesho ya biashara ya sabasaba yanayoendelea kwenye viwanja vya Mwalimu J.K. Nyerere Barabara ya Kilwa jijini Dar es salaam.
O
Afisa Mahusiano wa BANK OF AFRICA tawi la Tandika Bi. Beatrice Richard akihojiwa na mwandishi wa habari wa Radio EFM aliyetembelea katika banda hilo, kushoto ni Muganyizi Bisheko Bw. Muganyizi Bisheko Meneja Masoko/ Utafiti Maendeleo BANK OF AFRICA.
Afisa Mahusiano wa BANK OF AFRICA tawi la Tandika Bi. Beatrice Richard kulia Bw. Muganyizi Bisheko Meneja Masoko/ Utafiti Maendeleo wa BANK OF AFRICA katikati na Emmy Addie wakiwa katika picha ya pamoja kwenye banda lao.
Hapa wakifurahia jambo katika banda lao.
………………………………………………………………………
Bw. Muganyizi Bisheko Meneja Masoko/ Utafiti Maendeleo BANK OF AFRICA amewakaribisha wananchi kutembelea banda la maonyesho la benki hiyo lililopo namba 85 katika ukumbi wa Sabasaba Hall viwanja vya J.K.Nyerere ili kupata taarifa mbalimbali kuhusu huduma zinazotolewa na benki hiyo yenye matawi kadhaa jijini Dar es salaam na mikoani nchini Tanzania.
Akizungumza na Mtandao wa Fullshangweblog katika maonyesho hayo Bw. Muganyizi amewakaribisha wananchi kutembelea banda lao na matawi yake mbalimbali yaliyopo nchini ili kujipatia huduma mbalimbali za kibenki zinazotolewa na benki ya BANK OF AFRICA ili kujikwamua kiuchumi na kuwezesha maendeleo katika biashara zao.
Bw. Muganyizi amesema benki hiyo inatoa huduma mbalimbali ambazo ni Mikopo ya Uwekezaji katika Nishati Mbadala / Ufanisi wa Nishati, Ukodishaji wa Mitambo ya Uzalishaji mali (Lease Finance) Ujenzi wa Nyumba za gharama nafuu , Mikopo Midogo na ya Kati na Huduma mbalimbali za akaunti na huduma za kibenki kwa njia ya Kielektroniki
Bw. Muganyizi Bisheko Meneja Masoko/ Utafiti Maendeleo wa benki hiyo amewakaribisha wananchi wote katika banda lao ili kupata maelezo ya huduma mbalimbali zinazotolewa na benki hiyo, Ameongeza kwamba wao kama BANK OF AFRICA wanayo furaha kubwa kutumia fursa hii ya maonyesho ya Sabasaba wakiwa wanasherehekea miaka kumi ya benki hiyo kwepo kwake nchini Tanzania
Post a Comment