Header Ads

header ad

MAUZO SOKO LA HISA WIKI HII YATAKATA


Haya ndiyo yaliyojiri kwenye soko la hisa wiki iliyoisha Ijumaa tarehe 28 Julai 2017.
Mauzo ya Hisa (Turnover/ Liquidity)
Thamani ya mauzo ya  hisa kwa wiki hii yamepanda  mara tatu (3) zaidi kutoka Shilingi bilioni 4 wiki iliyopita hadi Shilingi bilioni 12.5 wiki hii iliyoishia tarehe 28 Julai 2017.

Vilevile pia idadi ya hisa zilizouzwa na kununuliwa imepanda kwa karibu mara nne Zaidi (4) kutoka hisa  milioni 14 wiki iliyoisha tarehe 21 Julai 2017, hadi hisa milioni 46 kwa wiki iliyoishia 28 Julai 2017.
Kampuni zilizoongoza katika mauzo ya hisa ni kama ifuatavyo:
CRDB     …………………………………………..……77%
TBL      ……..…….………………..…………..………22%
MKCB  …………..…….....……….……....………… 0.29%
Ukubwa Mtaji (Market Capitalization)
Ukubwa wa mtaji wa kampuni zilizoorodheshwa katika soko umeshuka kwa Shilingi Bilioni 595 kutoka Shilingi Trilioni 18.5 wiki iliyopita hadi Shilingi Trilioni 17.9 wiki iliyoishia tarehe 28 Julai 2017. Hii ni kutokana na kushuka kwa bei za hisa za Acacia (ACA) kwa 31% kutoka shilingi 7,430 hadi shilingi 5,100.
Ukubwa wa mtaji wa kampuni za ndani umeongezeka kwa Shilingi Bilioni 13 kutoka Shilingi Trilioni 7.70 wiki iliyopita hadi Shilingi Trilioni 7.71 wiki hii. Hii ni kutokana na kupanda kwa bei ya hisa za CRDB Bank kwa 2% kutoka shilingi 205 hadi shilingi 210.
Hati Fungani (Bonds)
Mauzo ya hati fungani katika wiki iliyoishia tarehe 28 Julai 2017 yamepungua kutoka Shilingi bilioni 35.2 wiki iliyopita hadi Shilingi Bilioni 1.4
Mauzo haya yalitokana na hatifungani kumi na sita (16) za serikali na za Makampuni binafsi                        (Corporate Bonds) zenye jumla ya thamani ya Shilingi bilioni 1.6 kwa jumla ya gharama ya Shilingi Bilioni 1.4.

Viashiria (Indices)
Kiashiria cha kampuni zilizoorodheshwa katika soko yaani DSEI kimepungua kwa pointi 68 kutoka pointi 2,134 hadi pointi 2,066 kutokana na kushuka kwa bei za hisa za kampuni mbali mbali zilizopo sokoni.
Kishiria cha kampuni za ndani yaani TSI kimepanda kwa pointi 6 kutoka pointi 3664 hadi pointi 3670, baada ya hisa za CRDB kupanda kwa 2% kutoka shilingi 205 hadi shilingi 210 wiki hii.
Kiashiria cha sekta ya viwanda (IA) kimebaki kwenye wastani wa shilingi 4793 kwa wiki hii.
huduma za kibenki na kifedha (BI) wiki hii kimepanda kwa pointi 17 kutoka pointi 2,615 hadi pointi 2,632 kutokana na kushuka kwa bei za hisa za kampuni mbali mbali zilipo sokoni
Kiashiria cha Sekta ya huduma za kibiashara (CS) wiki hii imebaki kama awali kwenye wastani wa shilingi 2475.

Shindano la Wanafunzi la Uwekezaji
Shindano la DSE SCHOLAR INVESTMENT CHALLENGE 2017 lilifika mwisho tarehe 30 Juni 2017. Zaidi ya wanafunzi wa vyuo na secondary 12,000 walishiriki katika shindano la mwaka huu, ikiwa ni Zaidi ya mara 3 ya mwaka uliopita, 2016.
Matokea ya washindi wa shindano hili yalitangazwa tarehe 18 July 2017 baada ya kufanyika tukio la mwisho la kuhusisha wanafunzi 10 bora kushiriki katika kipindi cha maswali na majibu na washindi  watatu (3) kuamuliwa na jopo ya majaji wa shindano hili.
Wafuatao ndio walio ibuka washindi wa shindano kwa Shule za Sekondari na Vyuo Vikuu.

DSE SCHOLAR INVESTMENT CHALLENGE 2017 WINNERS UNIVERSITIES
1
1ST WINNER
BENSON MCHARO
SOKOINE UNIVERSITY OF AGRICULTURE
2
2ND WINNER
FRANK JOHNSON
ARDHI UNIVERSITY
3
3RD WINNER
CHARLES MSONGE
SOKOINE UNIVERSITY OF AGRICULTURE
4
4TH WINNER
OMEGA EMMANUEL
SOKOINE UNIVERSITY OF AGRICULTURE
5
5TH WINNER
ZAKIA MIKIDADI YAHYA
INSTITUTE OF RURAL DEVELOPMENT


DSE SCHOLAR INVESTMENT CHALLENGE 2017 WINNERS SECONDARY SCHOOLS
1
1ST WINNER
IRENE PHARLES
SCHOLASTICA SECONDARY SCHOOL
2
2ND WINNER
CHRISTOPHER NGONYANI
KIBAHA BOYS SECONDARY SCHOOL
3
3RD WINNER
EMMANUEL ISACK MWENDA
KIBAHA BOYS SECONDARY SCHOOL



No comments

Powered by Blogger.