MAAGIZO YA WAZIRI MWIGULU KWA JESHI LA MAGEREZA HAYA HAPA
Waziri wa mambo ya ndani ya nchi ameagiza Jeshi la magereza mkoa wa Iringa kuanza mala moja Ndani ya mwezi mmoja ujenzi wa Gereza jipya la mkoa wa iringa kwani lilipo sasa linatakiwa kubomolewa.
Waziri Mwigulu mezungumza hayo akiwa ziarani mkoa wa Iringa kukagua Gereza hilo baada ya kupata taarifa kutoka kamati ya Ulinzi na usalama ya mkoa ikiongozwa na mkuu wa mkoa wa Iringa wakiomba Gereza hilo liondolewe mahala hapo kwani ipo karibu sana na Hospital ya mkoa hivyo kiusalama si mahali salama.
Waziri Mwigulu amesema anawapa mwezi mmoja kuandaa vifaa vitakavyotumika katika ujenzi wa gereza hilo na nyumba za askari huku akiwaambia kuwa wawatumie wafungwa katika ujenzi na kama hawatoshi basi wakawachukue mikoa ya jirani.
Mkuu wa magereza mkoa wa Iringa Afwelile mwakijungu amesema wasingependelea kuona mwingiliano wa wahalifu na wasio wahalifu hivyo wanaona gereza likiamishwa itakua salama zaidi na wanampango wakujenga gereza litakalochukua wafungwa zaidi ya elfu moja ukilinganisha sasa lina uwezo wakuchukua wafungwa zaidi ya 200 lakini hufikia hatua kuchukua mpaka miatano
Post a Comment