MANJI ‘ASOMEWA MASHTAKA SABA AKIWA KITANDANI’
HATIMAYE Mfanyabiashara mashuhuri Nchini ambaye pia alikuwa ni Mwenyekiti wa Klabu ya Yanga, Yusuph Manji na wenzake watatu wamesomewa mashtaka saba na Mahakama ya hakimu Mkazi Kisutu yakiwamo ya uhujumu uchumi na usalama wa nchi.
Mshtaka hayo walisomewa Kwenye Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete alipolazwa Mtuhumiwa namba moja Yusuph Manji Mbele ya Hakimu Mkazi wa mahakama ya Kisutu,Huruma Shahidi Wakili wa Serikali Kishenyi Mitalemwa aliyewasomea washtakiwa mashataka yao.
Watuhumiwa wengine ambao wapo katika kesi hiyo ni Pamoja na Abdala Sangey, Deogratias Kisimba, na Tobias Fwele
Shtaka la Kwanza ambalo watuhumiwa hao wamefunguliwa ni kosa la kukutwa na mabunda 35 ya vitambaa vinavyotumika kutengenezea sare za polisi zenye thamani ya milioni 192.5 mnamo 30 Juni 2017 katika eneo la chang’ombe Temeke Jijini Dar es Salaam.
Shtaka la Pili watuhumiwa wote Tarehe 30 Juni walikutwa na Mabando Manane ya vitaambaa zinazotumika kutengeneza JWTZ.
Kosa la Tatu watuhumiwa walikutwa na mihuri mbalimbali ya serikali hususani Jeshi la Tanzania iljyoandikwa “Mkuu wa kikosi 121 kikosi cha jeshi JWTZ” bila kuwa na uhalali wa kumiliki vitu hivyo kitendo kinachotarisha usalama wa nchi.
Kosa la Nne watuhumiwa walikutwa na Mhuri wa Serikali walikutwa na muhuri wa JWTZ yenye maandishi Kamanda kikosi 834 KJ makutupola Dodoma bila kuwa na uhalali kitendo ambacho kipo kinyume na sheria za Nchi.
Shtaka la tano kukutwa na Mhuri wa Serikali wenye maneno “COMMANDING Oficcer 835 kj Mgambo P.O.BOX…”
Shtaka la sita kukutwa na mali inayozaniwa kupatikana isivyo halali ambapo Tarehe 1 Julai katika eneo la Changombe, washtakiwa walikutwa na Plate namba SU 383 ambayo ilipatakana isivyo halali.
Washtakiwa Hawakuruhusiwa kujibu mashtaka hayo kwa sababu wanashtakiwa kwa sheria ya Uhujumu Uchumi na usalama wa taifa.
Hakimu Shahidi amesema Kwamba masuala hayo yasikilizwe kwenye Mahakama yenye mamlaka.
kesi hiyo itatajwa tena Tarehe 19 mwezi Julai na upelelezi wa Kesi haujakamilika.
kesi hiyo itatajwa tena Tarehe 19 mwezi Julai na upelelezi wa Kesi haujakamilika.
Post a Comment