MADIWANI WA CUF 19 WA DAR WATANGAZA KUMPINGA LIPUMBA
Madiwani 19 wa chama cha wananchi CUF wa Manispa za Mkoa wa Dar es Salaam wamempinga Profesa Ibrahim Lipumba na kutangaza kuunga mkono maamuzi ya viongozi wa chama hicho ya kufungulia kesi dhidi ya Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA) kwa madai ya wakala huo kusajili majina mapya ya wajumbe wa Bodi ya Wadhamini ya CUF pasipo kujiridhisha juu ya uhalali wa majina hayo.
Akizungumza Leo na wanahabari jijini dar es salaam Naibu Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Mussa Kafana amesema wanapinga juhudi zinazofanywa na Lipumba na wafuasi wake kwa madai kuwa zinalenga kuharibu taswira ya chama hicho kwa jamii na uvunjifu wa amani.
Aidha amesema kuwa wao kama Madiwani wa CUF wanaunga mkono hotuba iliyotolewa na Katibu Mkuu Maalim Seif pamoja na maamuzi ya viongozi kupinga maamuzi ya RITA mahakamani ambayo yamekiuka sheria ya wadhamini kifungu cha 26na wanaunga mkono pendekezo la chama hicho kuwasilisha mambo katika Mahakama Kuu ya kuitaka isimamishe kesi nyingine za CUF zilizofunguliwa hadi shauri linalohusu uhalali wa maamuzi ya RITA litakapoamuliwa.
Naye Naibu Meya wa Ilala, Omary Kumbilamoto amesema hakuna diwani miongoni mwao atakayekubali kuhojiwa na Kamati ya Maadili na Nidhamu ya Lipumba.
Msimao wa madiwani hao umekuja siku moja baada ya Profesa Lipumba ambaye ni Mwenyekiti wa CUF anayetambuliwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, kudai kwamba hakuna chombo chenye uhalali wa kuishitaki RITA mahakani kwani chama hicho hakikuwa na bodi halali tangu Agosti 2015.
Na James Salvatory
Post a Comment