WATUMISHI WATAKAOVUJISHA TAARIFA ZA SERIKALI WACHULIWE HATUA ZA KISHERIA"MAJALIWA"
Majaliwa Ameyasema Hayo Mjini Dodoma wakati Akizindua programu ya Mafunzo ya siku 5 ya uongozi kwa wakuu wa wilaya na Wakurugenzi kutoka mikoa 6 hapa nchini ambayo yanayotolewa na Taasisi ya Uongozi.
Sambamba na hayo, Waziri Mkuu ameongeza kuwa katika kipindi hiki cha utandawazi suala la utunzaji wa taarifa za serikali bila kuvuja pamoja na matumzi mazuri ya nyaraka ni muhimu kuzingatiwa.
Mh Majaliwa, amewataka viongozi kuonesha ushirikiano kwa wakuu wa wilaya na wabunge Pamoja na viongozi wa chini, na kwa yeyote atakaye kiuka sheria sheria ichukue mkondo wake.
sanjari na hayo, Mh Majaliwa amesema kuwa wapo baadhi ya viongozi ambao, wanao daiwa kutowaheshimu viongozi wao wakuu.
Akizungumza kwa niaba ya wakuu wa wilaya walioshiriki katika mafunzo hayo Mkuu wa Wilaya ya Dodoma mjini Bi.Christina Mndeme amesema kuwa wao kama viongozi wakotayari kufanya kazi wakati wowote bila kujali mazingira ya kazi.
Jacqueline Victor- SalvaNews
Post a Comment