TANZANIA HAIJAFIKIWA NA UGONJWA WA EBOLA “DKT MPOKI”.
NA ALLY DAUD-WAMJW
TANZANIA bado haijafikiwa na ugonjwa wa ebola kama inavyodaiwa na baadhi ya watu kutokana na utafiti uliofanyika na wataalamu
wa afya hapa nchini.
Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Mpoki Ulisubisya wakati wa mkutano na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam kuhusu tishio la uwepo wa ugonjwa huo katika nchi za jirani .
“Wananchi wanashauriwa kutokuwa na hofu bali wachukue tahadhari zaa kujikinga na ugonjwa huu kwani mpaka sasa hakuna mtu aliyethibitishwa kuugua ugonjwa huu hapa nchini” alisema Dkt. Ulisubisya.
Post a Comment