HOSPITAL YA AGA KHAN WAANZA UPASUAJI WA MIFUPA,NYONGA NA MAGOTI
Hospital ya Aga khan leo Mei 5, wameanza kufanya upasuaji wa mifupa ikiwemo wagonjwa wa nyonga na magoti ikiwa lengo ni kusaidia wananchi kupata huduma bora za matibabu kwa gharama nafuu na kuokoa gharama za kusafiri nje ya nchi kutibiwa.
Akizungumza na waandishi wa habari Leo jijini Dar es salaam Muuguzi Mkuu wa Hospitali ya Aga Khan, Lucy Hwai amesema kuwa Madaktari bingwa kutoka Hospitali ya Prince Aly Khan ya nchini India kwa kushirikiana na madaktari wa Aga Khan nchini watashirikiana na madaktari wa hospitali hiyo kufanya upasuaji kwa wagonjwa wa mifupa na nyonga kwa siku tatu
Aidha amesema ujio wa madaktari hao bingwa utakua endelevu na kwamba utasaidia kuongezea ujuzi madaktari wa hospitali hiyo ili mwakani ujenzi utakapo kamilika wagonjwa watapata huduma ya upasuaji pasipo kusafiri nje ya nchi na kuokoa gharama ikiwemo za usafiri.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Aga Khan, Sisawo Konteh amesema imepanga kuboresha huduma zake kwa kufanya mradi wa upanuzi wa hospitali unaogharimu dola za kimarekani milioni 80 utakaokamilika mwezi Juni mwaka 2017, kwa kujenga majengo ya wodi yatakayo beba vitanda 170.
Naye
Daktari Bingwa wa Mifupa na Majeruhi katika Hospitali ya Aga Khan, Harry Matoyo
amesema ujio wa madaktari bingwa hao ni muendelezo wa ushirikiano baina ya
hospitali shirika na Aga Khan ambao watashirikiana nao kufanya upasuaji wa
mifupa kwa kutumia teknolojia ya kisasa ikiwa pamoja na matumizi ya kompyuta.
Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Prince Aly Khan Sanjay Oak amesema lengo la ujio wao hapa nchini ni kuwawezesha madaktari kupata ujuzi ili kusaidia wananchi kupata huduma bora za matibabu kwa gharama nafuu na kuokoa gharama za kusafiri nje ya nchi kutibiwa.ya Aga khan leo Mei 5, wameanza kufanya upasuaji wa mifupa ikiwemo wagonjwa wa nyonga na magoti ikiwa lengo ni kusaidia wananchi kupata huduma bora za matibabu kwa gharama nafuu na kuokoa gharama za kusafiri nje ya nchi kutibiwa.
Na James Bayachamo-SalvaNews
Post a Comment