WAFANYAKAZI WA NMB KUCHANGIA UPASUAJI WA WATOTO WENYE MDOMO SUNGURA
Wafanyakazi wa Benki ya NMB katika kitengo cha Corporate
Support wamedhamini upasuaji wa watoto wanne wenye midomo Sungura
waliokuwa wamelezwa katika hospitali ya CCBRT jijini Dar es Salaam.
Akizungumzia udhamini huo, Meneja Mwandamizi wa Idara ya
Usimamizi wa Majengo NMB, Elizabeth Lukaza alisema ufadhili huo ni
sehemu ya utaratibu ambao wamejiwekea wao kama wafanyakazi wa kitengo
cha Corporate Support kusaidia jamii kwa sehemu yenye uhitaji.
Alisema ufadhili huo ulikuwa wa Dola 1,200 (Tsh. 2.6
milioni) na hiyo siyo mara ya kwanza wao kutoa ufadhili kwa kuchangia
huduma mbalimbali za kijamii kwani kila mwaka hufanya hivyo angalau mara
tatu.
Baadhi
ya wafanyakazi wa kitengo cha Corporate Support cha NMB, Meneja
Mwandamizi wa Idara ya Usimamizi wa Majengo NMB, Elizabeth Lukaza na
Meneja anayesimamia Mipango ya Maeneo ya Kazi, Faraja Rugusi wakifurahi
na mmoja wa watoto ambaye amefanyiwa upasuaji wa mdomo Sungura kwa
ufadhili wa wafanyakazi wa kitengo cha Corporate Support cha NMB,
Emmanuel Isdor, aliyekaa ni mama wa Emmanuel, Maines Ephrahim.
“Kila mwaka tunatoa msaada kwa jamii, kwa mwaka huu
tumekuja CCBRT tumesaidia watoto wanne ambao walikuwa wanatakiwa
kufanyiwa upasuaji wa mdomo Sungura, upasuaji wa kila mtoto tumetao
Dolla 300,
“Pesa hizi tumejichangisha katika kitengo na ofisi
imetuchangia sehemu ya fedha ili kufanikisha lengo letu, tumekuwa
tukifanya mambo mbalimbali, tumewahi hata kutoa damu kwenye kituo chao
kilichopo Mwananyamala,” alisema Elizabeth.
Pia alizungumzia mipango ya kitengo chao kwa siku zijazo, “Kuna
vitu vingi vya kufanya, kama kitengo chetu tumemuakuunga mkono juhudi
za benki kupitia kitengo cha masuala ya uwajikikaji kwa jamii (CSR) .
Pia tutaendelea kufuatilia maendeleo ya afya za watoto hawa kupitia
wazazi wao.”
Mmoja wa wanufaika wa ufadhili wa Emmanuel Isdor akiwa na mama yake Maines Ephrahim.
Nae mmoja wa wazazi ambao mtoto wake amefanyiwa upasuaji wa
mdomo Sungura kwa ufadhili wa NMB kupitia kitengo cha Corporate
Support, Maines Ephrahim alionyesha furaha na kuwashukuru NMB kwa
ufadhili huo na kueleza kuwa kabla ya upasuaji huo hali ya mtoto ilikuwa
tofauti na ilivyo sasa.
“Nawashukuru NMB kwa msaada ambao wamempatia mtoto wangu
(Emmanuel Isdor), amefanyiwa upasuaji vizuri … kabla ya upasuaji mtoto
alikuwa analialia, lakini sasa hali ni nzuri nimefurahi ,” alisema Maines.
Post a Comment