SAMIA AWATAKA WAKUNGA KUFANYA KAZI KWA BIDII
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Samia akihutubia Wakunga kwenye kilele cha Sherehe za Siku ya Wakunga Duniani
Wakunga wakirekodi hotuba ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan wakati wa sherehe za Siku ya Wakunga Duniani ambapo kitaifa zimefanyika mjini Dodoma.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akihutubia Wakunga waliojitokeza kwa wingi kwenye kilele cha Siku ya Wakunga Duniani ambayo Kitaifa imefanyika mkoani Dodoma na mgeni rasmi ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan.
Wakunga nchini wametakiwa kuhamasisha jamii kutumia huduma za uzazi wa mpango wakati wanapo tembelea jamii zao, Kutoa huduma kwenye cliniki za afya ya mama na mtoto,kwa akina mama wajawazito.
Hayo yamesemwa na makamu wa raisi wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania mh samia suluhu hasani ambaye ndiye aliye kuwa mgeni rasmi, wakati wa maadhimisho ya kilele cha siku ya mkunga duniani kitaifa yaliyo fanyika mjini Dodoma katika ukumbi wa chuo cha mipango yaliyo hudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali akimwemo waziri wa afya maendeleo ya jamii, jinsia wazee na watoto dk ummy mwalimu.
Bi samia ameongeza kuwa, serikali inakusudia kuhakikisha kuwa asilimia 50 ya vituo vya afya nchini vinavyo milikiwa na serikali vinatoa huduma kamili ya uzazi na za dharura,
Kwa upande wake waziri wa afya maendeleo ya jamii, jinsia wazee na watoto dkt ummy mwalimuameahidi kufanya kazi kwa bidii ili kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi, kuwataka wakunga kufanya kazi kwa kuzingatia weledi.
Nae rais wa chama cha wakunga Tanzania TAMA feddy mwanga, kwa niaba ya wakunga ameiomba serikali kuimarisha elimu ya wakunga hapa nchini kwa kutofautisha mkunga na muuguzi.
serikali kupitia wizara ya afya imetoa mwongozo wa kutaka kila kifo cha mama na mtoto kinachotokana na matatizo ya uzazi kijadiliwe ndani ya saa 24 katika kituo au hospitali husika kwa lengo la kubaini chimbuko la kifo na kuchukua hatua stahiki ikiwa ni pamoja na kuboresha zaidi kwa huduma zinazotolewa katika kituo husika.
Siku ya mkunga duniani huadhimishwa kila ifikapo may 5 ya kila mwaka na kauli mbiu ya mwaka huu “wakunga, akina mama na familia niwashirika wa kudumu”, ambayo kitaifa kwa mwaka huu yamefanyika mkoani hapa.
Watumishi wanne wa Halmashauri ya wilaya ya Nyang’hwale mkoani Geita wamerudishwa kazini baada ya kusimamishwa kwa miezi 4 kutokana na utovu wa nidhamu kazini.
Mkurugenzi mtendaji wa halimashauri ya Nyang’hwale Bw,Carlos Gwamagobe amesema miongoni mwa watumishi waliorudishwa ni pamoja na Muuguzi Linda Fransis ambaye alisababisha kifo cha mtoto mchanga.
Hata hivyo mkurugenzi amewataka watumishi hao kufanya kazi kwa uaminifu na kujitoa ili kuweka imani kwa wananchi na taifa kwa ujumla.
Post a Comment