Header Ads

header ad

WATUMISHI KUCHUKULIWA HATUA ZA KISHERIA KWA KUCHUA MISHAHARA HEWA



Na Jacqueline Victor- SalvaNews

Serikali ya Zanzibar haitasita kumchukulia hatua za kisheria mtumishi atakaebainika kushiriki au kuchukua mishahara hewa.

Kauli hiyo imetolewa na katibu mkuu kiongozi ofisi ya raisi Abdull-hamid Yahya Mzee wakati akizungumza na waandishi wa habari ikulu mjini Unguja.

Amesema tamko la rais kumtaka mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali kufanya ukaguzi katika idara zote za serikali kumebainika kuwepo mishahara na wafanyakazi hewa.



Katibu mkuu kiongozi huyo amebainisha kuwa kutokana na ukaguzi uliofanyika baadhi ya taasisi zimeanza kurejesha fedha zilizochukuliwa kinyume na sheria.



Pia Abdull-hamidamewataka watendaji wakuu wa taasisi za serikali kufuata sheria na taratibu zilizowekwa hasa katika suala la mishahara  kwani imekuwa ikiingizia nchi harasa kubwa.




No comments

Powered by Blogger.