MAFUNZO KWA VIKUNDI VYA UJASIAMALI KUWAWEZESHA KUJITAMBUA
Wanavikundi vya ushirika kupatiwa mafunzo ya uendeshaji kutawezesha wajasiriamali kujitambua na kufanya shughuli zao kwa kupata faida.
Kauli hiyo imetolewa na baadhi ya wajasirimali walioshiriki katika mafunzo ya siku tatu juu ya namna ya uendeshaji wa miradi yao yaliyoandaliwa na Fawehuko katika ukumbi waBen-bella Mjini Unguja.
Wamesema kupatiwa mafunzo kutawasaidia kufahamu mipango ya uendeshaji wa kazi zao katika vikundi na kuondokana na hasara walizokuwa wakizipata hapo awali.
Mwezeshaji wa mafunzo hayo kutoka Z.N.C.C.I.A Salma Salim Omar amesema kutolewa kwa mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo wa kuendesha shughuli zao kasa kwa kumsaidia mtoto wa kike.
Afisa elimu kutoka Wilaya ya Kaskazini A MShamara Chum Kombo amebainisha kuwa taasisi ya Fawe ina lengo la kuwasaidia wanawake na mtoto wa kike kupitia vikundi vyao vya ushirika.
Nae meneja mwendeshaji wa Fawe Wardati Mustapha Hamid amesema utoaji wa elimu ni muhimu katika kumsaidia mwanamke namna ya kuendesha shughuli zao ikiwa ni lengo la taasisi hiyo katika kuwasaidia wanawake.
Mratibu wa Fawe Zanzibar Hinda Abdallah Ajmy amesema kutokana na jukumu kubwa linalowakabili wanawake katika familia taasisi hiyo imeamua kuwawezesha ili kusimamisha vyema familia zao na kuondokana na changamoto zinazowakabili.
Post a Comment