TRL YAANZISHA SAFARI YA TREN YA MIZINGO DAR,DODOMA
Na James Bayachamo-Salvanews
Shirika la reli Tanzania (TRL) Leo Limeanzisha safari ya treni ya mizingo (FLAG OFF) ya shirika la mpango wa chakula duniani (WFP) lenye lengo la kuhudumia wateja kwa kiasi na muda unaoridhisha na kufikisha bidhaa kwa walaji wake.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo mapema Leo jijini dar es salaam mkurugenzi mtendaji wa TRA Masanja Kadogosa amesema kuwa kihistolia huduma hii ilikuwepo tokea enzi za shirika la reli Tanzania TRC na katika mwaka 2004 ilikuwa imeshasafirisha jumla ya tani 400,723 za WFP na kuanzia mwaka 2006 ukashuka tokea tani 66,994 hadi tani 846 tu mnamo mwaka 2015.
Aidha amesema kuwa moja kati ya changamoto iliyopo ni ukosefu wa vichwa vya Tren vya kutosha na mabehewa Hata hivyo baada ya kujipanga na kuihakikishia huduma zinakamirika kusafirishia tani 7000 za mahindi kupeleka katika ghala kuu la WFP iliyoko Kiota Dodoma .
Kwa upande wake mwenyekiti wa bodi ya TRL John Kondoro amesema kuwa tangu mwaka 2000 hii ni Mara ya pili shirika hilo linasafirisha mizigo na kwa sasa wamesafirisha mzigo mkubwa na hii ikiwa ni faida maana inaongeza faida kwa shirika na kwa kufika hatua hiyo imani kubwa inajengeka kwa wadau kwa kazi hii inayofanyaka.
Post a Comment