MAJALIWA AWATAKA MABALOZI WA TANZANIA KUTANGAZA FURSA ZA UWEKEZAJI NCHINI
Waziri mkuuKassim Moajaliwa amekutana na mabalozi wa Tanzania wanaenda kuiwakilisha Tanzania katika nchi mbalimbali kuhakikisha wanaimarisha uhusiano na kujenga urafiki kati ya nchi wanazowakilisha kwa lengo la kuitangaza Tanzania kiuchumi,ikiwa ni pamoja na kueleza fursa za uwekezaji na utalii zilizopo nchini.
Mabalozi wa Tanzania walioteuliwa hivi karibuni na rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ,kuwakilisha Tanzania nnje ya
Nchi,wamefika ofisi ya waziri mkuu mjini Dodoma kwa lengo la kumuaga na
kwenda kuanza majumukumu yao katika nchi walizopangiwa.
Waziri mkuu amewaleeza mabalozi hao kuwa Tanzania inazo
fursa nyingi za uwekezaji Na jukumu lao la kwanza la Mabalozi hao ni
kuvitangaza vivutio vilivyopo ili kuleta wawekezaji wengi TANZANIA .
Suala la ushirikishwaji sekta binafsi pia waziri mkuu amesema Tanzania imelipa kipaumbele
Waziri Mkuu alizungumzia sula la watanzania waishio nje
ya nchi , aliwataka Mabalozi kuwakutanisha na kufanya nao mikutano mara
kwa mara ilikujua kama wanamatatizo yanayoyapata katika nchi wanazoishi
ilikuangalia jinsi gani wanaweza kusaidiwa,
Mabalozi hawa wanaenda kuiwakilisha Tanzania katika nchi za QATAR,UBELIGIJI,AFRIKA KUSINI,UJERUMANI,COMORO, ALGERIA,INDIA NA ,SUDAN.
Post a Comment