Header Ads

header ad

RAIS MAGUFULI KUZINDUA BARAZA LA TATU LA TAIFA LA BIASHARA



Na James Bayachamo-Salvanews
Rais magufuli anatarajia kuzindua baraza la tatu la taifa  la  biashara sambamba na kufungua mkutano wa baraza hilo na sekta binafsi  likiwa na lengo la kujadili fursa za uwekezaji katika sekta ya viwanda na biashara hapa nchini

Akizungumza na wandishi wa habari leo jijini dar es salaam Katibu Mtendaji, Baraza la Biashara la Taifa(TNBC) Raymond Mbilinyi amesema kuwa mkutano wa baraza hilo na sekta binafsi unatarajia kufanyika mei 6 mwaka huu  kwa ajiri ya majariliano ambayo yatakuwa yanalenga ukuuaji wa mabadiliko ya viwanda  na namna ya kukuza viwanda na ushiriki wa secta binafsi katika kukuza viwanada nchini na kwa mkutano huu utawezesha kuweka ukaribu kati ya sekta binafsi na serikali

Aidha amesema kuwa  juhudi  bado zinafanyika kuhakikisha tunaboresha mazingira ya bishara hapa nchini  na kuna kamati iko chi ni ya waziri mkuu ili kuwezesha kuangalia maboresho ya kibiashara hapa nchini.


Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa sekta binafsi  (TPSF) Godfrey  Simbeye ameipongeza serikali ya awamu ya tano kwa kukuza sekta binafsi na kushirikiana nayo ili kuhakikisha Tanzania inafanikisha Sera ya uchumi wa viwanda huku akiwataka  wakuu wa mkoa na wakuu wa wilaya kuendesha mabaraza ya mikoa na wilaya ili kuwezesha kukutana na watu wa sekta binafsi ili kuhakikisha kila mkoa mpaka wilaya inakuwa na viwanda.


Wandishi wa habari hawakichukua taarifa hiyo



No comments

Powered by Blogger.