Header Ads

header ad

CHAKUA WATAKA MFUMO WA KI-ELEKTRONIKI



Chama cha Kutetea Abiria Nchini(CHAKUA)kimeitaka Serikali kuharakisha kuweka mfumo wa Ki-elektroniki kwenye Vituo vya Mabasi ili kusaidia kudhibiti ukataji wa tiketi Feki unaofanywa na Baadhi ya Mawakala wa Mabasi yaendayo Mikoani.

Akizungumza na Wanahabari leo Jijini Dar es salaam M wenyekiti wa CHAKUA Taifa Hassani Mchanjama amesema kuwa kwa sasa kumeibuka udanganyifu wa kuuziwa tiketi Feki kwenye kituo Kikuu cha Mabasi Ubungo jijini Dar es salaam(UBT).


Aidha amewatahadhalisha wananchi kuwa makini na ununuaji wa tiketi mitaani huku akiwasisitiza kufika katika ofisi za Kampuni za Mabasi katika Stendi Kuu ili kukata tiketi,kwani  hali hiyo itasaidia kuepukana na matapeli wanaowakatia tiketi kwa udanganyifu.


Kwa Upande wake Mkurugenzi wa CHAKUA Kanda ya MasharikiWilson Damo amewaomba wanahabari kuendelea kushirikiana na Chama hicho kutoa Elimu kwa Wanachi ili kudhibiti udanganyifu unaoendelea wa kuuza tiketi Feki.


 Na  James Bayachamo-Salvanews

No comments

Powered by Blogger.