Header Ads

header ad

WATU SABA WASHIKIWA NA JESHI LA POLISI KWA TUHUMA ZA KUVAMIA MKUTANO WA CUF

Watu saba wa CUF- upande wa profesa Ibrahim    Lipumba wanashikiriwa na jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es salaam kwa tuhuma za kuhusika na tukio la kuvamia Mkutano wa  wafuasi wa CUF upande wa Maalimu Seif Sharif Hammad  nakuwashambulia kwa kuwapiga katika hoteli ya Vinna April 22 mwaka huu.
Mbali na Watu hao Saba,pia Jeshi la Polisi kanda maalumu ya Dar es salaam linawashikiria watu wawili wa upande wa Maalimu Seif kwa kosa la kumshambuli aMohammed Mgomvi  ambaye ni Mlizni wa Profesa  Lipumba nakumkata kisigino ambapo kwa sasa anaendelea na matibabu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili(MNH).

Hayo yamebainishwa leo na Kamishna wa Kanda hiyo Simon Sirro wakati akizungumza na Waandishi wa habari kwa ajili ya kutoa ufafanuzi juu ya hatua zilizochukuliwa hadi sasa na Jeshi hilo,nakwamba watuhumiwa hao waliyokamatwa ni pamoja na Mkurugenzi wa Habari  CUF- Upande wa Profesa LipumbaBw.Abdul Kambaya.

Katika hatua Nyingine Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es salaamu limepinga ombi la CUF – upande wa Maalimu Seif  la kufanya usafi katika Ofisi za Makao Makuu ya Chama hicho Buguruni jijini Dar es salaam,ambao ulipangwa kufanyika Siku ya Jumapili ya Aprili 30 mwaka huu  kwa madai kuwa kunaviashiria vya uvunjifu wa amani.

Kufuatia tukio la Wafuasi waProfesa Lipumba kuvamia Mkuatano wa Wafuasi wa Upande wa  Maalimu Seif Aprili 22 mwaka huu Mabibo,lilisababisha kupigwa kwa baadhi ya waandishi wa habari ambao walikuwa wamealikwa kwenye mkutano huo na kuharibu vitendea kazi,kitendo ambacho kimelaaniwa vikali na wadau mbalimbali wa habari hapa Nchini.

 Na James Salvatorysaba wa CUF- upande wa profesa Ibrahim    Lipumba wanashikiriwa na jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es salaam kwa tuhuma za kuhusika na tukio la kuvamia Mkutano wa  wafuasi wa CUF upande wa Maalimu Seif Sharif Hammad  nakuwashambulia kwa kuwapiga katika hoteli ya Vinna April 22 mwaka huu.
Mbali na Watu hao Saba,pia Jeshi la Polisi kanda maalumu ya Dar es salaam linawashikiria watu wawili wa upande wa Maalimu Seif kwa kosa la kumshambuli aMohammed Mgomvi  ambaye ni Mlizni wa Profesa  Lipumbanakumkata kisigino ambapo kwa sasa anaendelea na matibabu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili(MNH).

Hayo yamebainishwa leo na Kamishna wa Kanda hiyo Simon Sirro wakati akizungumza na Waandishi wa habari kwa ajili ya kutoa ufafanuzi juu ya hatua zilizochukuliwa hadi sasa na Jeshi hilo,nakwamba watuhumiwa hao waliyokamatwa ni pamoja na Mkurugenzi wa Habari  CUF- Upande wa Profesa LipumbaBw.Abdul Kambaya.

Katika hatua Nyingine Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es salaamu limepinga ombi la CUF – upande wa Maalimu Seif  la kufanya usafi katika Ofisi za Makao Makuu ya Chama hicho Buguruni jijini Dar es salaam,ambao ulipangwa kufanyika Siku ya Jumapili ya Aprili 30 mwaka huu  kwa madai kuwa kunaviashiria vya uvunjifu wa amani.

Kufuatia tukio la Wafuasi waProfesa Lipumba kuvamia Mkuatano wa Wafuasi wa Upande wa  Maalimu Seif Aprili 22 mwaka huu Mabibo,lilisababisha kupigwa kwa baadhi ya waandishi wa habari ambao walikuwa wamealikwa kwenye mkutano huo na kuharibu vitendea kazi,kitendo ambacho kimelaaniwa vikali na wadau mbalimbali wa habari hapa Nchini.

 Na James Salvatory

No comments

Powered by Blogger.