NAMNA AMBAVYO UPOTEVU WA MAJI UNAVYOTOKEA KWA BAADHI YA MAENEO JIJINI DAR ES SALAAM
Aidha mwandishi wetu alishudia wananchi wakipita maeneo hayo na kuangalia upotevu huo huku wakiwa wanapita tu bila ya kudhibiti maji hayo ambapo mwandishi aliamua kuchukua jukumu la kufunga bomba moja kwa kamba ili kunusu angalia maji yalioyokuwa yakitililika kwa wingi.
Kwa upande wao baadhi ya wananchi wa mtaa huo waliojitambulisha kwa majina ya Agnes Eric na debora wameiambia Salvanews kuwa ni wiki sasa tangu maji hayo yakitilika pasipo kuona jitihada zozote za utengenezwaji mambomba hayo ambayo wamedai mara baada ya mvua kunyesha na mkondo mkubwa wa maji kupita mabomba hayo yalikatika
Kwa mujibu wa afisa mtendaji mkuu wa shirika la maji safi na maji taka Dar es salaam (DAWASCO)mhandisi Cyprian Luhemeja katika ziara ya Katibu mkuu wa wizara ya maji na umwagiliaji profesa Kitila Mkumbo alisema kuwa changamoto kubwa shirika hilo linalokabiliana nazo ni pamoja na upotevu mkubwa wa maji unatokana na uchakavu wa miundo mbinu ya maji ikiwemo mabomba ya kusafirishia maji hayo kwenda kwa watumiaji pamoja na wizi wa maji unaofanywa na baadhi ya wananchi wasio waaminifu na wamefanya jitihada mbali ikiwemo uboreshaji ili kuhakikisha upotevu huo wa maj unapungua na hatimaye kumalizika kabisa ambapo kwa sasa umepungua kutoka asilimia 57 mwaka 2015 na kufikia asilimia 37.8 mwezi march mwaka huu.
Eneo ambalo inadaiwa Mara baada ya mvua kunyesha mabomba mawili yalikatika na kupelekea kumwagika maji
Bomba ambalo mwandishi alilifunga kwa kwamba aliyoipata maeneo hayo hayo na kushibiti maji kwa muda huo
Bomba ambalo lililokatika mara baada ya mvua kunyesha na kupelekea upotevu wa maji
Na James Bayachamo-Salvanews
Post a Comment