WAZIRI MKUU AKAGUA MAKAZI YA MAKAMU WA RAIS
WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa amekagua matengenezo ya makazi ya muda
yanayotarajiwa kutumiwa Makamu wa Rais, Mhe. Samia Suluhu Hassan pindi
atakapohamia Dodoma.
Waziri Mkuu amefanya ukaguzi huo leo mchana (Jumatano, Desemba 6, 2017) katika eneo la Kilimani, mjini Dodoma ambako yalikuwa makazi ya Mkuu wa Mkoa huo.
Akitoa
taarifa ya ujenzi huo, Waziri wa Nchi (OWM) anayeshughulikia Sera,
Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira, Wenye Ulemavu na Vijana, Bibi Jenista
Mhagama alisema Kikosi kazi cha kuratibu zoezi la Serikali kuhamia
Dodoma kilibaini kuwa mahali alipokuwa akiishi awali siyo sahihi kwa
ajili ya makazi ya kudumu ya Mhe. Makamu wa Rais.
“Pale
palikuwa panafaa kwa ajili ya ziara za kikazi alipokuwa akija Dodoma,
kwa hiyo tumeamua tufanye ukarabati hapa, ili aweze kuishi kwa viwango
vinavyostahili.”
Alisema
kazi ya matengenezo kwenye makazi yake itagharimu sh. bilioni 1.5
wakati kazi ya kutenganisha ofisi za watumishi na wasaidizi wa Makamu wa
Rais itagharimu sh. milioni 680.
Waziri Mkuu pia alikagua matengenezo ya Ofisi inayotarajiwa kutumiwa na Makamu wa Rais ambayo itakuwa eneo la Ndejengwa.
Wakati huohuo, Kaimu
Meneja wa TBA Mkoa wa Dodoma, Bw. Steven Simba ambaye anasimamia ujenzi
huo, alimweleza Waziri Mkuu wanataraji kuwa kazi hiyo itakamilika kabla
ya Desemba 30, mwaka huu.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
S. L. P. 980,
41193 – DODOMA.
Post a Comment