MPINA AITAKA KAMPUNI YA GAME TRACKING SAFARIS KUONDOKA KWENYE RANCHI YA UVINZA
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mh.Luhaga Mpina akizungumuza na Meneja wa Kampuni ya Game
Tracking Safaris(TGTS) Audax Kalulama katika simu alipotembelea Ranchi ya
Uvinza leo na kuamuru mwekezaji huyo kuondoka kabla ya Januari Mosi mwakani
kutokana na Mwekezaji huyo kukaa katika eneo hilo kinyume cha Sheria.
Waziri wa
Mifugo na Uvuvi Mh.Luhaga Mpina (katikati) kitoa maamuzi ya kuitaka Kampuni
ya Game Tracking Safaris(TGTS) kuondoka
katika eneo la hekta 20000 kwenye vitalu
tisa vilivyomo kwenye Ranchi ya
Uvinza ifikapo tarehe 1/1/2018.
Sehemu ya Ranchi ya Uvinza.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mh.Luhaga Mpina (katikati) akiwasikiliza walinzi wa Kampuni ya Game Tracking Safaris(TGTS)
hawapo pichani wakitoa maelezo alipotembelea Ranchi ya Uvinza leo.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mh. Luhaga Mpina ameutaka uongozi wa Kampuni ya Game Tracking Safaris(TGTS) kuangalia na kupitia nyaraka walizonazo ili kuona uhalali wa umiliki wa eneo la hekta
20000 kwenye vitalu tisa vilivyomo
kwenye Ranchi ya Uvinza inayomilikiwa na
Kampuni ya Ranchi za za Mifugo za Taifa (NARCO)kabla ya Selikali kuwatoa
kwa nguvu ifikapo tarehe 1/1/2018.
Waziri Mpina ametoa
maelekezo hayo leo alipotembelea Ranchi
ya Uvinza kuangalia shughuli mbalimbali
katika Ranchi hiyo ambapo ametoa muda wa hadi Januari mosi mwakani kwa mwekezaji huyo kuondoka katika eneo hilo endapo atabaini kuwa amekuwa akikaa kimakosa kuanzia
katika vitalu namba 41 hadi 49.
Aidha Waziri Mpina amesema
endapo Mwekezaji huyo ataendelea kubaki
baada ya tarehe Mosi Januari, Serikali itamuondoa kwa nguvu na atatakiwa kulipa gharama zote za fidia na usumbufu.
“Ninakuagiza angalia
taarifa mbalimbali ulizonazo
kuhusu umiliki wa eneo hili kama
utaona umeendelea kukaa
hapa bila kufuata taratibu
tafadhali uondoke mara mmoja ili kupisha
Serikali kuendelea na shughuli zake” alisisitiza Mpina
Waziri Mpina
amemuagiza Meneja Mkuu wa NARCO, Profesa
Philemoni Wambura kuwaandikia barua ya
kuwaondoa wawekezaji wote katika Ranchi hiyo ambao hawajaendeleza kwa zaidi ya
asilimia 40 na kwamba wawekezaji ambao
wamewekeza kwa zaidi ya asilimia arobaini wanatakiwa kukamilisha malipo yote
kabla ya Januari mosi mwakani.
Alionya wawekezaji kuacha tabia ya kuidanganya serikali
kwamba wanauwezo wa kuwekeza katika vitalu
ili wapewe lakini wanabadili matumizi baada ya kupewa. Aliongeza
kwamba Serikali imegundua baadhi ya wawekezaji wanaopewa vitalu wanawakodisha
wafugaji kutoka nchi jirani na kujipatia
faida wakati Serikali haipati chochote.
Awali, Meneja wa (TGTS) Audax
Kalulama akizungumza kwa simu na Waziri Mpina kutoka Arusha amesema
kwamba eneo hilo wanamiliki kihalali na kuomba muda ili wawasiliane na
Wizara ya Mifugo kuonyesha taarifa
za umiliki wa eneo hilo.
Post a Comment