HOSPITAL YA AGAKHANI YAFUNGUA HOSPITALI NYINGINE KIGAMBONI
Hospitali ya Aghakani imeombwa kupunguza gaharama za matibabu ili huduma zao za afya zinazokuwa kwa kasi ncini ziweze kuwafikia wananchi wenye vipato vidogo
Hayo yamesemwa leo jijini dar es salaam na Katibu tawala wa wilaya ya kigamboni Rechel Muhando wakati wa uzinduzi wa hospitali ya 11 ya Aghani kwa mkoa wa dar es salaam ambayo iko kigamboni ambapo amesema kuwa kuziduliwa kwa hospitali hiyo kutasaidia kuimarisha afya za watanzania na kuongea ajira ambapo mpka sasa ajiri 15 za moja kwa moja zimepatikam hali ambayo inachangia kufikia nchi ya viwanda kwani watanzania wakiwa na na afya njema wataweza kufanya kazi
Aidha amesema kuwa kufunguliwa kwa kituo hicho kutapunguza mrudikano wa wagonjwa katika hospitali zingine na kuwapunguzia wananchi kutembea umbali mrefu kwenda kutafuta huduma za afya.
Kwa upande wake mkurugenzi uendeshaji wa vituo vya Agakhani Tanzania Fayyaz Mohamedamesema kuwa hospitali hiyo itakuwa ikitoa huduma na gharama sawa na hospitali za agakhani zilizopo kote nchini ambapo kituo kitakuwa na huduma za kawaida na huduma za mama na mtoto
Naye mkurugenzi wa uguuzi wa hospitali hiyo Lucy Hwai amesema kuwa Kwa sasa wanaendelea kuboresha mfumo wa afya jumuishi nchini nzima na wanaendeleza upanuzi wa hospitali kuu ya agakhani unayogharimu shilingi billion 176 ambapo ikikamilika itasaijidia jamii na serikal katika sekta ya afya
Insert: Hwai
Kufikia mwaka 2020 Hospitali ya Agakhani imejipanga kuwa na hospitali 35 nchi nzima hali ambayo itasaidia kutoa huduma za afya kwa taifa
Na James Salvatory
Post a Comment