LHRC YASEMA NA SERIKALI KUHUSU UCHAGUZI WA MADIWANI
Kituo
cha sheria na haki za binadamu (LHRC) kimeitaka serikali pamoja na vyombo vya dola kufanya uchunguzi wa kina na kuchukua hatua kali za kisheria kwa wote watakaobainika kuhusika kwa namna moja au nyingine katika uvunjifu wa haki za binadamu katika uvurungu zilizotokea wakati wa Uchaguzi wa Madiwani wa kata 43 uliofanyika jumapili nchi nzima.
Pia Kituo hicho kimeitahadharishwa serikali kuwa kama isipokemea vitendo hivyo vya uvunjifu wa Haki za Binadamu ,kutasababisha athari mbaya kwenye uchaguzi wa serikali za Mitaa utakaofanyika 2019 pamoja na uchaguzi mkuu wa mwaka 2020.
Akizungumza na Waandishi Habari leo Jijini Dar es Salaam wakati wa kutoa tathmini ya Uchaguzi huo ,Kaimu Mkurugenzi wa (LHRC),Anna Henga, amesema kituo hicho kimefuatilia kwa ukaribu uchaguzi mdogo wa marudio wa kuchagua madiwani katika kata 43 zilizopo halmashauri takribani 36 kwenye mikao 19 nchini na kubaini uchaguzi ulikuwa na kasoro lukuki zilizochangia uvunjifu wa haki za kibinadamu
Kwa upande wake mwanasheria wa kituo hicho bwana Wiliamu KahaleAmesema pamoja na ukweli kwamba baadhi ya kata uchaguzi ulifanyika kwa uhuru na haki lakini bado wamebaini pia uchaguzi huo ulitawaliwa na matukio ya watu kutekwa na watu wasiojulikana ,watu kupigwa ,kukamatwa na kujeruhiwa kwa lengo la kuharibu na kuvuruga uchaguzi na kuwatia hofu wapiga kura.
Katika uchaguzi mdogo wa marudio wa kuchagua madiwani katika kata 43 zilizopo halmashauri takribani 36 kwenye mikao 19 nchin Chama Cha Mapinduzi (CCM) kilishinda kata 42 huku Chadema ikiambulia ushindi wa kata moja.
Na James Salvatory
Post a Comment