‘FREE SUGAR’ YALETA MATUMAINI MAPYA KWA WAGONJWA WA KISUKARI.
Meneja wa Masoko Kampuni ya ABACUS Pharma Jeremiah Bwana.
Na Noel Rukanuga.
Kampuni ya ABACUS Pharma imefanikiwa kuleta ahuweni kwa watu wenye matatizo ya kisukari hapa nchini baada ya kuzindua bidhaa ya ‘Free Sugar’ ambayo inawapa fursa watanznia wote kutumia bidhaa hiyo bila kupata madhara yoyote ya kiafya.
Free Sugar ni bidhaa mpya ya sukari ambayo inawapa fursa wagonjwa wa kisukari na watanzania wote kuweza kutumia sukari hiyo yenye radha sawa na sukari ya kawaida bila kupata matatizo ya kiafya.
Akizungumzia bidhaa hiyo ya ‘Free Sugar’ Meneja wa Masoko Kampuni ya ABACUS Pharm Jeremiah Bwana, amesema kuwa free sugar ni sukari isiyokuwa na Calories (Calories 0%) jambo ambalo linawapa nafasi watanzania kunufaika na free sugar.
Amesema kuwa uwepo wa free sugar itawapa furaha watu wenye matatizo ya kisukari ambao muda mrefu wamekuwa hawatumii sukari ya kawaida kutokana na matatizo ya kiafya.
“italeta ahuweni kwa wagonjwa wa kisukari ambao awali walikuwa hawatumii sukari, lakini sasa itakuwa rafiki kutokana free sugar ina radha sawa na bidhaa nyengine” amesema Jeremiah.
Hata hivyo imeeleza kuwa uwepo wa ‘free sugar’ ni muhimu sana kutokana ugonjwa kisukari hapa nchini ni mkubwa sana, kwani Tanzania inashika nafasi ya tano duniani katika nchi ambazo wananchi wake wanaumwa ugonjwa wa kisukari.
Kutokana na mabadiliko ya tabia ya nchi pamoja na kula vyakula ambavyo sio rafiki kwa binadamu imeelezwa ni miongoni mwa sababu zinazosababisha kuongezeka kwa ugonjwa kisukari.
Familia nyingi zimekuwa zikitumia asilimia 25 katika pato lake kwa ajili ya kumuhudumia mgonjwa wa kisukari kitu ambacho gharama hiyo ni kubwa sana.
Akizungumza katika uzinduzi wa bidhaa ya Free Sugar, Mkuu wa Kitendo Cha Kisukari kutoka Hospitali ya Taifa ya Muhimbili Dk Mohamed Juma, amesema kuwepo kwa bidhaa ya free sugar itaweza kusaidia katika kutatua changamoto kadha zilizokuwepo hapa nchini.
Amesema kuwa bidhaa hiyo ni nzuri kwani radha yake nipo sawa na sukari ya kawaida katika mtumizi yoyote ambayo mtumiaji amekusudia kutumia.
“kutokana na umuhimu wa uwepo wa bidhaa ya free Sugar itasaidia kutatua changamoto ambazo zipi katika kufanikisha kuondoa matatizo ambayo yamekuwa kwa muda mrefu” amesema Dk Mohamed.
Hata hivyo Mratibu wa kisukari Wilaya ya Ilala, Daktari Bigwa Dk Bushara Faraja, amesema free sugar ni msaada mkubwa kwa wagonjwa ambao wanaumwa ugonjwa kisukari.
Amesema kuwa baada ya kuja bidhaa ya free Sugar kutoka Kampuni ya ABACU wataendelea kutumia sukari bila kupata madhara yoyote ya kiafya na kutofauti na awali.
“Bidhaa ya Sugar free ni nzuri kwani inampa mtu yoyote fursa ya kuweza kutumia bila kuingiza kitu chochote mwilini mbacho sio rafiki” amesema Dk Faraja
Post a Comment