YALIYOJIRI KATIKA MSAKO WA CD FEKI DAR
Kampuni ya Udalali ya Msama Auction Mart kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi,
Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) na Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na
Michezo imeendelea na zoezi la ukamataji wa Wadurufu wa kazi za sanaa na
wakwepa kodi kupitia kazi hizo.
Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) na Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na
Michezo imeendelea na zoezi la ukamataji wa Wadurufu wa kazi za sanaa na
wakwepa kodi kupitia kazi hizo.
Zoezi hilo limeendelea katika sehemu mbalimbali za jiji la Dar es Salaam ambapo pia imesisitizwa kuendelea nchi nzima.
Akizungumza na Waandishi wa
Habari kabla ya kuanza kwa shughuli hiyo, Mkurugenzi wa Msama Auction
Mart amewaasa Wafanyabiashara wote kufuata taratibu
kuhakikisha wanauza bidhaa zenye Stika ya TRA.
“Uzeni bidhaa zenye Stika ya TRA, acheni kuwaibia Wasanii, wakati huu ni wakati wa
Serikali kupata haki yake na Wasanii pia wapate haki zao,wafaidi jasho
la kazi yao”, amesema Msama
Pia amewaasa Watanzania
wanaonunua kazi hizo za sanaa kuacha kununua kazi ambazo hazina Stika
ya TRA, amesema Watanzania wanapaswa kujifunza kulipa Kodi kupitia kazi
hizo zenye Stika halali ya TRA.
“Wale wanaoburn CD,
Wanaoingiza nyimbo kutumia Kompyuta muache, zoezi hili sio Dar es Salaam
pekee zoezi ni la nchi nzima na tutahakikisha kila anayenunua bidhaa
hizo ananunua bidhaa zenye Stika”, amesisitiza Msama.
Post a Comment