WATOTO MILLIONI 15 HUZALIWA NJITI DUNIANI
Imeelezwa kuwa zaidi ya watoto milioni 15 Dunian huzaliwa kabla ya muda wake wa kuzaliwa wiki ya 32 ,33 wakatika kwa kawaida ni wiki 40 (watoto njiti) huku Tanzania ikiwa ni miongoni mwa nchi zinazokabiliana na tatzo hilo hali ambayo inasababisha vifo pindi mtoto asipopata huduma husika
Hayo yamesemwa na mkurugenzi wa hospitali ya agakhani Dkt Ahmed Jasabam wakati akizungumza na wandishi wa habari jijini dare s salaam katika hafla ya kuadhimisha siku ya mtoto njiti ambapo amesema kuwa watoto wanaozaliwa kabla ya wakati wake huwa wanahitaji uangalizi wa hali ya juu ikiwemo mahali penye joto , uwepo wa maziwa ya mama yenye vipimo maalumu na mahali salama pa kuwahifadhia
Kwa upande wake afisa wa kitengo cha magonjwa yasiyo ya kuambukiza kutoka wizara ya afya maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto Dkt, Mariam Kalomoamesema kuwa bado kuna changamoto katika baadhi ya hospitali hasa vituo vya afya (ZAHANATI), kutokutoa huduma kwa watoto jiti huku juhudi za serikali zikiendelea kuchukuliwa ili kuweza kufanikisha swala hilo
Lea Hevili ni mmoja kati ya wazazi waliojifungua mtoto njiti ameiambia Salvahabari kuwa yeye alijifungua mtoto mwenye miezi sita na alikutana na changamoto kadha, ikiwemo mtoto wake kuugua magonjwa, lakini baada ya kupata matibabu, mtoto wake alipona na kwa sasa ana umri wa miaka mitatu
Siku ya mtoto njiti huadhimishwa kila novemba 17 ya kila mwaka duniani wakati kwa mwaka huu hospitali ya agakhan iliadhimisha novemba 25
Post a Comment