WATANZANIA WAOMBWA KUCHANGIA DAMU
Wito umetolea kwa watanzania kuchangia damu ili kusaidia kuokoa maisha ya watanzania wenye uhitaji wa damu katika hospitali zetu
Wito huo umetolewa na mkurugenzi mtendaji wa amaana benki muksin salimu Katika kuadhimisha miaka 6 ya benki ya hiyo, ambapo wafanyaKazi wa benki hiyo wamefanya zoezi la uchangiaj i Damu kwa lengo la kuokoa maisha ya wahitaji Damu waliopo hospitalini.
Aidha amesema kuwa zoezi la uchangiaji limefanyika katika matawi yote ya benki yaliyopo dar es salaam, mwanza na arusha yameshiriki zoezi hilo ambapo matarajio ni kuchangia chupa za Damu zaidi ya mia moja.
Naye afisa wa muhamasishaji Marium juma kutoka mpango wa taifa wa Damu salama kanda ya mashariki amebainisha kuwa bado kuna uhaba mkubwa wa upatikanaji wa Damu salama hospitalini kwani Damu iliyopo haikidhi mahitaji ya mwaka kwa matibabu.
Post a Comment