WADAU WAKUTANA KUJADILI MALEZI YA WATOTO
Mashirika na Taasisi mbalimbali za kimataifa wamekutana nchini Tanzania kwa ajili ya kujadili namna ya kuwekeza kwa watoto katika malezi makuzi ili kutatua changamoto zinazowakabili.
Meneja Mradi wa Taasisi ya (AKU-IED, EA) kutoka nchini Kenya Leonard Falex, |
Akizungumzia mkutano huo,Mkurugenzi wa Huduma za Kinga kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dkt. Neema Rusibamayila amesema kuwa kuna mambo mengi ambayo wanapaswa kufanyiwa kazi ili tupige hatua.
Amesema kuwa ili kuhakikisha wanapiga hatua katika kufanyikisha makuzi ya watoto, malezi ushirikianao unaitajika.
“Kupitia mkutano huu tutajadili namna gani tunaweza kufanikisha makuzi ya watoto, lishe pamoja na malezi yanakuwa bora kwa watoto” amesema Rusibamayila.
Meneja Mradi wa Taasisi ya Maendeleo na Elimu ya Afrika Masharikiya (AKU-IED,EA) kutoka nchini Kenya Leonard Falex, amesema kuwa mkutano huo, kwa ajili ya kuwekeza kwa katika maisha ya watoto wachanga.
Amesema kuwa katika kufaniksha mpango huo mkutano umewakutanisha wadau mbalimbali ambapo watapata fursa ya kuulizana maswali pamoja na kushauriana ili kufikia malengo.
Falex amefafanua kuwa mkutano huo umeanza leo Oktoba 6 mwaka huu mpaka oktoba 9 mwezi huu.
“Wadau kutokana nchini tofauti wamekutana katika mkutano kwa ajili ya kujadili pamoja na kuwekeza katika maisha ya watoto wachanga ambao wameonekana wanaitaji msaada katika kufaniksha maisha yao” amesema Falex.
Mkutano huo ambao umeitishwa
na shirika la kuhudumia watoto Duniani (UNCEF) kwa kushirikiana na shirika la
afya Duniani( WHO)umewakutanisha wadau mbalimbali ikiwemo Taasisis ya Maendeleo
ya Kibinadamu ya Chuo Kikuu cha Aga Khan, vyuo na mashirika
yasiyoyakiserikali, wawakilishi kutoka nchi mbalimbali ikiwemo Zambia ,Kenya na
Uganda pamoja na wataalamu mbalimbali wa afya.
Post a Comment