WABUNGE WA CUF WALIOVULIWA UANACHAMA WAMUANDIKIA BARUA SPIKA WA BUNGE
Akizungumza na wanahabari mapema leo kwa niaba ya wabunge wenzake nane walivuliwa uanachama ndani ya chama hicho,Aliyekuwa Kiongozi wa Wabunge wa CUF BungeniRiziki Mngwali amesema kwamba wamemwandikia barua Novemba 20 mwaka huu Spika wa Bunge Jobu Ndugai wakimtaka kuchukua hatua ya kuwarejesha Bungeni kwana maamuzi ya mahakama yaliyotolewa hivi karibuni bado yanawatambua ni wabunge na wanachama halali hata hivyo bado hawajapata majibu yoyote kutoka kwake.
Aidha Mngwali ambaye pia alikuwa mbunge viti maalumu halmashauri ya Mafia amesema kuwa baada ya Mwenyeki Taifa wa Cuf anayetambuliwa na Msajili wa vyama vya siasaProf.Ibrahim Lipumbakuwavua unachama na kuteua majina mengine nane ya wabunge wa viti maalumu na kuyawasilisha kwa spikaNdugai ambaye hata hiyvo aliwaapisha bila kusubiri maamuzi ya mahakama kufuatia shauri dogo waliloliwasilisha katika mahaka kuu kanda ya Dr e salaam.
Itakumkukwa kuwa Julai 25,2017 Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzanian Job Ndugaialitangaza kuwavua ubunge wabunge nane na baadae tume ya uchaguzi NEC kuwatangaza wabunge wengine wapya wakushika nafasi hiyo kutoka upande wa Prof. Lipumba,
Wabunge waliyovuliwa ubunge wao ni Minza Bakari Haji,Savelina Silvanus Mwijage,Salma Mohamed Mwassa,Raisa Abdallah Mussa.
Wengine ni Riziki Shahari Mgwali,Khadija Salum Ally Al-qassmy,Halima Ali Mohamed pamoja na Saum Heri Sakala.
Na James Salvatory
Post a Comment