Header Ads

header ad

MADAKTARI SABA KWENDA INDIA KUJIFUA KUHUSU INI



Hospitali ya taifa ya muhimbili inatarajia kusafirisha wataalam saba kwenda nchini India kwa lengo la kupata mafunzo ya upasuaji wa kupandikiza ini na kuwaongezea uwezo wataalamu wa magonjwa ya ini nchini.

Akizungumza Jijini Dar es salaam mkuu wa kitengo cha mawasiliano kwa umma wa hospitali ya taifa ya Muhimbili Aminiel Aligaesha amesema kuwa wataalamu hao wanatarajiwa kuondoka hapa nchini Novemba 29 mwaka huu na wanatarajiwa kurudi nchini mwezi March 2018.

Aidha Aligaesha amesema mafunzo hayo yanalenga kutimiza azma ya serikali ya awamu ya tano kwa vitendo katika kupunguza rufaa za nje ambazo serikali ilikuwa ikigharimu fedha nyingi kutokana na kutokuwepo kwa wataalamu wa kutibu magonjwa hayo.

Kwa upande wake Mkuu wa kitengo cha magonjwa ya inni na mfumo wa chakula idara ya tiba hospitali ya Taifa ya muhimbili Dakta John Rwegasha  amesema matarajio yao ni kuhakikisha malengo ya utoaji wa tiba ya magonjwa ya ini yanafikiwa ili kuweza kuokoa vifo visivyo vya lazima.

Naye Daktari Bingwa wa mfumo wa chakula na iniMasolwa   Mwanasai ambaye ni mmoja wa baadhi ya wanaotarajia kusafiri hapo kesho kuelekea  nchini India kwa ajili ya mafunzo hayo amesema anaimani mafunzo hayo yatawaongezea uwezo zaidi katika upandikiza ini.


Katika kuhakikisha uboreshaji wa huduma za matibabu katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili,hospitali hiyo imekuwa ikihakikisha inakuwa inapata wataamu waliobobea katika utoaji wa huduma za magonjwa mbalimbali.

Na James Salvatory

No comments

Powered by Blogger.