Header Ads

header ad

TFDA YAZINDUA MAABARA HAMISHIKA ZIPATAZO 10


Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimuwa, akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Maabara Hamisika(Minlab Kits) 





Waziri wa Afya, Mandeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu, akizungumza wakati wa uzinduzi wa Maabara Hamishiki (Minlab Kits) jijini Dar es Salaam.






Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Chakula na Dawa Hiiti Sillo  akkizungumza wakati wa uzinduzi wa Maabara Hamishika jijini Dar es Salaam .





Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akipatiwa maelezo juu ya Maabara Hamishika.









Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) imezindua Maabara Hamishika (Minlab Kits) nyingine 10 zenye thamani ya sh. milioni 100 na kufanya idadi yake kuwa 25z zikiwa na lengo la 

kudhibiti dawa duni na bandia nchini 



Akizungumza leo jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi huo Mkurugenzi Mkuu wa TFDA Hiiti Sillo, amesema kununuliwa kwa maabara hizo kunatokana na mafanikio yaliyokwisha patikana kupitia mpango huo na kwa lengo kuongeza idadi ya sampuli za kuchunguza, ameeleza kila maabara imegharimu sh. milioni 10.

"Ongezeko la maabara hizi  litaongeza idadi ya vituo vya uchunguzi na kuimarisha ufuatiliaji wa ubora wa dawa katika soko," amesema Sillo.




Aidha ameeleza kuwa hatua hiyo inadhihirisha kwamba Mamlaka imejidhatiti katika kutekeleza majukumu yake ya kulinda afya ya jamii dhidi ya madhara yatokenayo na matumizi ya dawa duni na bandia.


Abainisha kuwa maabara hizo zitapelekwa katika ofisi tatu za kanda za TFDA ambazo ni Tabora (Magharibi), Mbeya (Nyanda za Juu Kusini) na Mtwara (Kusini).



Amesema nyingine zitapelekwa katika vituo vituo vya forodha vya Namangan a uwanja wa ndege wa Kimataifa wa KIA ( Kanda ya Kaskazini), Sirari na Mtukula (Kanda Mashariki) na nyingine zitapelekwa katika hospitali za mikoa ya Geita na Katavi.



Kwa upande wake Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimuwa ameitaka Menejimenti ya Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) kuendelea kujenga uwezo wa wataalam wa maabara wanaohusika na uchunguzi kupitia Maabara Hamishika (Minlab Kits) ili kuendana  na mabadiliko ya Sayansi na Teknolojia.


“Naitaka Menejimenti ya TFDA iendelee wataalamu wa maabara wanaohusika na uchunguzi kupitia maabara hizi ili kuendana na mabad liko ya Sayansi na Teknolojia,” amesema Waziri Ummy.


Aidha ameipongeza TFDA kwa kuendeleza mpango wa uchunguzi wa awali wa dawa ulioanza mwaka 2012 katika baadhi ya hospitali za Mikoa na Vituo vya forodha.


Amebainisha kuwa mpango huo unahusu uchunguzi wa dawa muhimu za kifua kikuu, dawa za kufubaza virusi vya ukimwi (ARVs), dawa za malaria pamoja na vijidudu (antibiotics).


Waziri Ummy akizungumza kuhusu maabara hizo, amesema ni hatua ambayo inalenga kuimarisha nguvu katika uchunguzi wa haraka na wa awali wa dawa (preliminary screeming tests) na hivyo kudhibiti ubora na usalama wa dawa zinazoingia nchini na zilizoko katika soko.


Amesema ni imani yake kuwa TFDA itahakikisha kwamba maabara hizo zinapelekwa katika vituo vilivyopangwa na kutumika kulingana na mpango wa ufuatiliaji wa ubora wa dawa nchini.


Aidha amewataka watakaozitumia kuhakikisha wanazitumia kama ilivyokusudiwa ili ziweze kukaa muda mrefu.




No comments

Powered by Blogger.