MARUFUKU KUINGIA MAKUBALIANO NA NGO BILA KUPITA TAMISEMI"NZUNDA"
TIGANYA VINCENT- RS-TABORA
SERIKALI imepiga marufuku Halmashauri zote nchini kuingia makubaliano na Mashirika yasiyokuwa ya kiserikali(NGO’S) bila kupitia na kiuhidhinishwa na Ofisi ya Rais , Serikali za Mitaa na Tawala za Mikoa( TAMISEMI ) kwa kuwa baadhi ya mambo yamekuwa hayaendebi na vipaumbule vya Serikali ambayo nakusudia kuwasaidia kuwasaidia wananchi.
Kauli hiyo imetolewa jana mjini Tabora na Naibu Katibu Mkuu (ELIMU) Ofisi ya Rais , Serikali za Mitaa na Tawala za Mikoa( TAMISEMI ) Tixon Nzunda wakati akizungumza na Watendaji na watumishi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Manispaa ya Tabora , Halmashauri za Wilaya ya Sikonge, Uyui , Kaliua na Urambo.
Alisema kuwa kabla ya kuanza utekelezaji wa shughuli za NGO ni vema Halmashauri zikapeleka maombi ya mashirika ambayo yameomba kufanyakazi katika maeneo yao ili Serikali inone kama kweli inaendana na vipaumbele ambavyo imepanga katika kuboresha maisha ya watanzana ambao maisha yao yako chini.
Nzunda alisema mashirika hayo yamekuwa yakidai pesa ya kusaidia Watanzania kutoka kwa wafadhili lakini matokeo yake fedha hizo zimekuwa zikiishi kuwanufaisha watu wachache na wanapoaandika taarifa kwa watu waliowapa fedha wadai kuwa wamewasaidia Watanzania katika miradi ya maendeleo ya mabilioni ya fedha kumbe sio kweli imeshia mifukoni kwa wachache.
Alisema kuwa Serikali ya Awamu ya Tano inelenga kuhakikisha kuwa kama fedha zinatolewa kwa ajili ya walemgwa ziende kusaidia eneo husika ili kuhakikisha thamani ya fedha inaonekana kwa jami husika , kwa Serikali na wafadhili na wafadhili husika.
Nzunda alisema kuwa kumekuwepo na mashirika ambapo yamekuwa yakutumia mbinu ya kuwasaidia wananchi kumbe fedha hizo zimekuwa zikiwanufaisha watu wachache kwa kulipwa posho na mambo mengine ambayo hayana tija kwa wananchi wa kawaida.
Alisema Mashirika amabayo yana nia ya kweli ya kusaididia watanzania lazima yakubaliane na viapumbe vya Serikali ili yaweze kufanya kufanya kazi nchini vingine ni vema yakatafute nchini nyingine ya kufanya mambo yake bila kufuata utaratibu wa nchi hisika.
Nzunda alitoa wito kwa Halmashauri ya kuhakikisha kuwa kabla ya kuyaruhusu Mashirika hayo yamepata kibali cha TAMISEMI ili kuepuka kisingizio cha kuwageuza wananchi mtaji wa wache kujipatia fedha kwa maslahi binafisi.
Alisema mashirika yamekuwa yakianda taarifa nzuri kwa wanawapa fedha kuwa wamesaidia jamii husika kumbe hakuna kinachoonekana Zaidi ya wao kunufaika
Nzunda alisema kuwa Halmashauri itakayoingia makubaliano ya NGO bila kupitia TAMISEMI watendaji wake itabika wawajibishwe kwa kusimamia maslahi ya umma.
Naibu Katibu Mkuu yupo katika ziara ya kikazi katika Mikoa ya Kigoma, Tabora na Singida kwa lengo ya kuhimiza usimamizi bora wa sekta ya elimu , kilimo, mifugo , utawala bora na mengine mengi.
Post a Comment