HII HAPA NEEMA KWA WALEMAVU WA DAR
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam akipokea mchango kwa ajili ya walemavu wa miguu leo.
Hawa ni baadhi ya walemavu wakifanya mazoezi baada ya kuwekewa mguu bandia katika hospitali ya CCBRT iliyopo Msasani jijini Dar.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mh. Paul Makonda amewataka wananchi pamoja na wadau mbalimbali kujitokeza kwa wingi katika kuchangia miguu bandia kwa ajili ya Walemavu wa miguu,ili kurejesha furaha na tumaini jipya kwa waliokatwa miguu kutokana ajali au ugonjwa wa kisukari.
Amesema uhitaji wa miguu bandia ni mkubwa kwani watu wamekwatwa miguu kutokana an ajali au ugonjwa wa kisukari,hivyo serikali pamoja na wadau mbalimbali tunaomba wananchi waweze kujitokeza kuchangia ili kurudisha furaha na amani kwa walemavu ili kurudi katika maisha yao kama mwanzo na kuendelea na kazi zao walizokuwa wakifanya
"Natamani kwenye msimu huu wa kwenda kufunga mwaka we we uliye salama kumrudishia furaha na amani kwa kuchangia MTU mmoja na kuleta matumaini kwa watu wa Mkoa huu wa Dar es Salaam wenye uhitaji huu wa miguu bandia" Amesema
Ameishukuru Hospital ya CCBRT kwa kuunga mkono kampeni hiyo pamoja E FM RADIO na TV E walioojitolea kuhamasisha jamii kuchangia Miguu Bandia.
"Account namba ya kuweza kuchangia yenye jina "Uchangiaji wa Miguu bandia Dar es Salaam" Namba 0150299713500 wananchi wote wanaweza kuweka hela kokote kule na niendelee kuomba tena ni ihari yako kuweza kuwarejeshea matumaini wenzetu walipata ulemavu wa miguu kwa ajali au kutokana na ugonjwa wa kisukari". Amesema Makonda
Vilevile amesema kuwa atazungumza na Taasisi zinazotoa Bima ya Afya ili waongeze kipengele cha Matibabu na kutoa Miguu bandia kwa watu waliopoteza Miguu kwa Ajali au Ugonjwa.
Kwa upande wake Afisa mwendishaji Mkuu wa hospitali ya CCBRT Brenda Msangi amesema wao walishirikiana na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kuwasaidia walemavu wa miguu na wamechangia kampeni hiyo kwa kuwasaidia watu 35 na tayari wamepataiwa miguu walemavu 21 ambapo amewataka wadau mbalimbali pamoja na wananchi kujitokeza kwa wingi kuchangia kwani uhitaji bado ni mkubwa.
Katika hatua nyingine Makonda amepokea kiasi cha Shillingi Million 10,000,000 kutoka kampuni ya Ujenzi ya SPECTUM DESIGN ambapo Mkurugenzi wake Arch.JIMMY MKENDA amesema lengo la kutoa mchango huo waliwiwa na kuamua kujumuika kuchangia kampeni hiyo inayolenga kuwasaidia waliokata tamaa baada ya kupoteza miguu waweze kurejesha furaha na amani kwa hawa waliopata ulemavu kutokana na ajali au ugonjwa wa kisukari.
Gharama za mguu mmoja wa bandia kwanzia matengenezo hadi kukamilika unagharimu shilingi milioni 1.5 kwa waliopata ajali na kukatwa miguu na waliokatwa miguu kwa Ugonjwa wa kisukari gharama yake ni milioni 4.5 hadi milioni 4.7 kwanzia unapotengenezwa hadi kukamilika na mtu kupatiwa mguu huo.
Post a Comment