SERIKALI PWANI YAONYA WAHALIFU WENYE MAJERAHA KUTIBIWA KINYEMELA
Mkuu wa mkoa wa Pwani Mh. Injinia Evarist Ndikilo akizungumza na wananchi huko Kibiti na Ikwiriri.
Baadhi ya wananchi wakimsikiliza Mkuu wa mkoa wa Pwani Mh. Injinia Evarist Ndikilo.
…………………………………………………………………………………
Na Mwamvua Mwinyi,Kibiti
MWENYEKITI wa ulinzi na usalama mkoani Pwani,mhandisi Evarist Ndikilo,amewaonya waganga wa zahanati ,vituo vya afya ,ama mtumishi wa afya na maduka binafsi ya dawa wilayani Kibiti na Rufiji kuacha kujihusisha kuwatibia wenye majeraha yasiyoeleweka ikiwemo risasi wasiowajua bila kupata taarifa kamili kutoka polisi .
Amesema atakaebainika kutibia watu wa aina hiyo hatosita kuchukuliwa hatua za kisheria.
Aidha ,mhandisi Ndikilo ,ameeleza waliokuwa wakidaiwa kujihusisha na vitendo vya kiuhalifu na mauaji wilayani humo wengi wao wametiwa nguvuni .
Katika hatua nyingine ,mkuu huyo wa mkoa ,amewataka wenyeviti wa Vijijini na vitongoji kuitisha mikutano ya mapato na matumizi kuanzia sasa kwani hali ni shwariii.
Akizungumza na wakazi wa Ikwiriri na Kibiti ,alisema matibabu yatolewe kwa mtu mwenye taarifa kutoka vyombo husika kwani wapo baadhi ni wahalifu wanaotaka kutibiwa kinyemela.
Alisema vyombo vya dola bado vinaendelea na mapambano ,kazi ya kudhibiti inaendelea hadi hapo watakapojiridhisha.
Mhandisi Ndikilo, alibainisha kwamba ,kuhusu katazo la kutumia usafiri wa pikipiki kuanzia saa 12 jioni ,bado linaendelea ,ni marufuku usafiri huo kwa muda huo .
“Vijana wetu madereva bodaboda najua mnategemea kipato kwenye usafiri huu lakini tuvumilieni kidogooooo ,kidogoooo muda mdogo umebaki tutaruhusu lakini bado Kwanzaa”
“Tunahitaji kujiridhisha kama wahalifu waliokuwa wakiondoa amani yetu ,wamekamatwa ” alisema mhandisi Ndikilo.
Aliwasihi baadhi ya wananchi na viongozi mbalimbali waliohama wilayani humo kwa kuogopa hali ya sintofahamu iliyokuwepo warejee kuendelea na shughuli zao.
Alieleza kuwa ,hivi karibuni kulikuwa na hofu na shaka kwa baadhi ya wawekezaji na wananchi kwa hali ya usalama wao hasa katika wilaya ya Rufiji na Kibiti.
“Nami nasisitiza kama mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama mkoa vyombo vya dola vimefanikiwa kudhibiti waliokuwa wanaua ovyo,hivyo wananchi walioondoka warudi “alisema mhandisi Ndikilo. .
Kwa mujibu wa mwenyekiti huyo ambae pia ni mkuu wa mkoa wa Pwani,kulisitishwa mikusanyiko ya watu ,mikutano ya hadhara ya vijiji na vitongoji lakini kwasasa iendelee .
Mhandisi Ndikilo, alitoa wiki mbili mikutano hiyo ianze kuitishwa ,wananchi wanahitaji kujua fedha zao zimetumiwajwe .
Nae kamanda wa kamanda maalumu Rufiji,kamishna msaidizi mwandamizi Onesmo Lyanga,alisema wananchi wanapaswa waelewe kilichopigwa marufuku ni kutumia usafiri wa pikipiki saa 12 jioni.
Usafiri huo hauruhusiwi kuanzia muda huo na sio watu kuacha kuendelea na shughuli zao za kibiashara ama kutembea.
Usafiri huo hauruhusiwi kuanzia muda huo na sio watu kuacha kuendelea na shughuli zao za kibiashara ama kutembea.
Kamanda Lyanga ,alisema wanaendelea kushirikiana na wananchi vizuri na amewaomba endapo kuna jambo ama viasharia vya kiuhalifu wasisitize kutoa taarifa polisi.
Aliwatoa hofu watu wote wanaofanya shughuli zao kwenye wilaya hizo kutokuwa na wasiwasi ,ulinzi umeimarishwa .
Kamanda Lyanga ,alisema wamewashughulikia waliobainika kufanya mauaji na uhalifu katika ukanda huo .
Post a Comment