Header Ads

header ad

MAJIBU YA TANESCO KUHUSU KUBOMOLEWA KWA JENGO LAO LA UBUNGO

 TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI 
Uongozi wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO)  unapenda Vyombo vyote vya Habari vifahamu kuwa Tumepokea Agizo la Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Joseph Magufuli, kuhusu Kubomolewa  kwa Jengo la Ofisi za TANESCO  Makao Makuu, liliopo Ubungo Jijini Dar es salam, 
Tunapenda Watanzania watambue kuwa TANESCO inaungana na Mheshimiwa Rais katika jitihada zake za kuleta Maendeleo katika nyanja mbali mbali, hivyo TANESCO itatekeleza Agizo hili ndani ya muda ulio pangwa.
Tunapenda kuwahakikishia Wateja wetu na Watanzania wote kwa ujumla kuwa katika utekelezaji wa Agizo  hilo , Huduma za umeme zitaendelea kupatikana kama  kawaida, ikumbukwe kuwa ni wajibu wa kila Mtanzania kuunga mkono jitihada zinazo fanywa na Mheshimiwa Rais.
Uongozi wa Shirika unajipanga kutekeleza Agizo la Mheshimiwa Rais, Tunaomba Vyombo vyote vya Habari vitoe nafasi kwa Shirika kukamilisha taratibu hizi. Tutaendelea kutoa taarifa Zaidi kila inapo bidi. 
                         TANESCO ‘‘Tunayaangaza Maisha yako’’ 
Kwa mawasiliano
Mitandao ya Kijamii
www.facebook/tanescoyetu

Imetolewa Na:  OFISI YA UHUSIANO
                               TANESCO- MAKAO MAKUU.
                                Novemba 17, 2017

No comments

Powered by Blogger.