Header Ads

header ad

MAAGIZO KWA WANAFUNZI KUHUSU MAKUMBUSHO


  Balozi wa Denmark Bw.Einarh Jensen ambae alikuwa mgeni rasmi katika onesho hilo akizungumza na wadau waliohudhuria.  

wasanii wa ngoma wakisherehesha kwenye maonyesho hayo
Na Helena Matale Dar es salaam
Wanafunzi wa vyuo ,sekondari,pamoja na shule za msingi wametakiwa kujijengea tabia ya kutembelea Makumbusho ili kujifunza na kuziendeleza fursa mbalimbali ambazo zilikuwa zinafanywa hapo awali ili kujipatia kipato na kukuza uchumi wa nchi.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Makumbusho Prof. Audax Mabula alipokuwa akizungumza katika maonyesho ya picha ya "Karibu Tanzania"yaliyofanyika Leo Makumbusho ya Taifa  ambapo amewataka vijana kutembelea 

Makumbusho kwa kusema kuna  wataweza kujifunza vitu mbalimbali kupitia picha ambazo zilipigwa miaka 50 iliyopita zikionyesha shughuli mbalimbali walizokuwa wakizifanya ambapo hivi Sasa hazitiliwi mkazo hali yakuwa zinafaida kubwa kwa Taifa kiujumla"Alisema MABULA.

Hata hivyo Prof.Mabula ameongeza kwa kusema kuna umuhimu mkubwa kwa vijana wa nchi hii kufatilia mambo yaliyofanywa hapo awali kama kufinyanga,kuchonga na kutengeneza dhana mbali mbali kwa ajili ya kilimo ili kujikwamua kiuchumi hivyo kupitia jumba la maonyesho la Makumbusho ya Taifa wataweza kujifunza hivyo vyote.

Pia amesema wataweza kuzijua asili zao kiundani kwani wataweza kujifunza tamaduni za kwao kwa kutumia picha mbalimbali zilizopo hivyo kuna haja kubwa ya kutembelea Makumbusho.

Kwa upande wake Balozi wa Denmark ambae alikuwa mgeni rasmi katika onesho hilo la picha Bw.Einarh.Jensen amesema kuna haja kubwa ya kujifunza vitu vinavyohusiana na asili zetu kwani vina tija hivyo amewaasa vijana zaidi kutembelea makumbusho kujifunza kwa nadharia kwani wao ndio muhimili mkubwa katika kila Taifa.

Pia kwa upande wa  wanafunzi waliohudhuria katika onesho hilo waliotokea shule ya Baobab wamesema kuwa  wamefurahi kushiriki katika onesho hilo kwani wamejifunza vitu vingi ikiwemo kuona namna watu wa zamani walivyokuwa wakijikwamua kiuchumi kupitia shughuli za kilimo,uhunzi na vinginevyo huku nyenzo yao kubwa ikiwa ni mikono yao.

No comments

Powered by Blogger.