MAAGIZO MAZITO ALIYOYATOA RAIS MAGUFULI KWA WAMILIKI WA VIWANDA
Rais
John Magufuli ametoa siku 14 kwa wamiliki wa kiwanda cha nguo cha
Mwatex cha jijini Mwanza na cha dawa cha Keko jijini Dar es Salaam
kuonyesha mpango madhubuti wa kiutendaji na uendeshaji.
Amesema kinyume cha hilo, viwanda hivyo vitataifishwa na kurejeshwa kwenye umiliki wa umma.
Rais
Magufuli amesema hayo leo Jumanne Oktoba 31,2017 alipozungumza na
wananchi baada ya kuzindua kiwanda cha dawa za binadamu cha Prince
Pharmaceutical eneo la Buhongwa jijini Mwanza.
Amesema
Serikali imechoka kusikia kauli na maelezo ya “tuko kwenye mchakato”
zinazotolewa kama kinga kwa viwanda visivyofanya kazi kwa kiwango
kinachostahili.
Rais
ametoa agizo hilo baada ya kupokea taarifa kuwa kiwanda cha Mwatex
kinafanya kazi kwa asilimia 20 ya uwezo wake wa uzalishaji.
Akizungumzia
ujenzi wa kiwanda cha dawa, Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu amesema
utawezesha mikoa ya Kanda ya Ziwa kuwa na uhakika wa upatikanaji wa dawa
kwa bei nafuu.
Mwalimu
amesema katika utekelezaji wa Tanzania ya viwanda, wizara kwa
kushirikiana na wadau wanakamilisha mchakato wa kujenga kiwanda cha
dripu na bidhaa zingine za hospitali mkoani Simiyu.
Kuhusu
uboreshaji wa huduma za afya, amesema Mkoa wa Mwanza umepokea zaidi ya
Sh7.1 bilioni kwa ajili ya kununua vifaa tiba na dawa.
Post a Comment