Header Ads

header ad

KESI YA TUNDU LISSU YAUNGURUMA



Na mwandishi wetu
KESI ya uchochezi inayomkabili mbunge, Tundu Lissu na wahariri wa gazeti wa la Mawio imeahirishwa hadi Novemba 30, 2017 kwa sababu Lissu anaumwa. Washtakiwa wengine wote walikuwapo.


Tundu Lissu
Kesi hiyo ipo katika hatua ya usikilizwaji wa ushahidi wa mashahidi wa upande wa mashtaka kwa Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba.

Leo wakili wa serikali, Elizabeth Mkunde  amedai kesi ilipangwa kwa ajili ya kutajwa na akaomba ipangiwe tarehe nyingine ya kuitaja.

Hakimu Simba ameahirisha hadi Novemba 30, 2017. Washtakiwa  wengine wanaokabiliwa na kesi hiyo  ni Mhariri wa gazeti la Mawio, Simon Mkina, Jabir Idrisa na Mchapishaji wa Kampuni ya Jamana, Ismail Mehboob.

Lissu na wenzake  Simon Mkina, Jabir Idrisa na Mchapishaji wa Kampuni ya Jamana, Ismail Mehbooh wanakabiliwa na mashtaka matano ikiwamo la kuandika habari za uchochezi kinyume na Sheria ya Magazeti ya Mwaka 2002.

Inadaiwa kuwa Januari 12 hadi 14, 2016 katika jiji la Dar es Salaam, washtakiwa watatu, Jabir, Mkina na Lissu, kwa pamoja waliandika na kuchapisha taarifa‎ za uchochezi zenye kichwa cha habari kisemacho, ‘Machafuko yaja Zanzibar’.

Katika shtaka la pili wanadaiwa kuwa Januari 14, 2016 katika jiji la Dar es Salaam, walichapisha habari hizo ili kuleta chuki kwa wananchi wa Zanzibar.

Mshtakiwa Mehboob anadaiwa kuwa Januari 13,2016 katika jengo la Jamana lililopo Manispaa ya Ilala,  Dar es Salaam, alichapisha gazeti la Mawio lililokua na taarifa za uchochezi.

Alidai mshtakiwa huyo pia  alichapisha gazeti hilo bila ya kuwasilisha hati ya  sheria ya kiapo kwa Msajili wa Magazeti.

Mbali na mashtaka hayo washtakiwa hao kwa pamoja wanadaiwa kuwa Januari 14, 2016, Dar es Salaam, bila ya kuwa na mamlaka yoyote, waliwatisha na kuwatia hofu wananchi wa Zanzibar   wasiweze kuingia kwenye marudio ya Uchaguzi Mkuu.

No comments

Powered by Blogger.