KATA ZINAZOONGOZA KWA KUTIRIRISHA MAJI TAKA MJINI KAHAMA
Kata za Kahama mjini, Majengo, Malunga, Nyihogo na Mhungula katika halmashauri ya Mji wa Kahama mkoani Shinyanga, zimetajwa kuongoza kwa kutiririsha maji ya vyooni wakati wa mvua hali inayohatarisha maisha ya wananchi.
Akizungumza na Kijukuu Blog, Mkuu wa idara ya Usafi na Mazingira Halmashauri ya Mji wa Kahama, MARTINE MASELE amesema Idadi kubwa ya wanaotozwa faini ama kufikishwa mahakamani kwa kosa la kutiririsha maji machafu ni kutoka katika kata hizo.
Ili kudhibiti hali hiyo, MASELE amewataka wananchi kuendelea kushirikiana na serikali kuwabaini wanaohusika na utiririshaji wa maji machafu katika mitaa yao ili hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yao.
Amesema jumla ya Watu 36 wamefikishwa mahakamani mwaka huu kwa kosa la kutiririsha maji machafu na kwamba idadi kubwa ya wananchi wanapigwa faini kwa makosa ya usafi wa mazingira katika maeneo yao.
MASELE amewataka wananchi kuwa msatari wa mbele kuwafichua wanaotiririsha maji katika maeneo yao na kwamba kwa kufanya hivyo itasaidia kuweka mazingira katika hali ya usafi muda wote.
Post a Comment