Header Ads

header ad

WAZIRI MWIJAGE AZINDUA KITUO CHA USAMBAZAJI VIFAA VYA UJENZI NCHINI




Jumla ya  dola milioni 75 za kimarekani  zinatarajiwa kujenga  majengo matatu ya usambazaji bidhaa za ndani nchini,  chini ya kampuni ya uuzaji wa vifaa vya ujenzi kutoka China (NBMG).



Akizungumza leo katika uwekaji wa jiwe la  msingi eneo la Tabata-Matumbi jijini Dar es Salaam ,Waziri wa Viwanda na Biashara, Charles Mwijange, amesema kuwa kituo  hicho kitakuwa kikisambaza vifaa vya ujenzi na  kitawasaidia Watanzania kujipatia ajira na kuongeza ufanisi kwa vijana nchini kwa kunufaika na kituo hicho huku akiwaomba wawekezaji hao kuangalia jinsi wanavyoweza kuongeza uzalishaji wa mihogo, pamba na utengenezaji wa nguo kwa sababu maeneo yote hayo bado yanatafuta wawekezaji.

Aidha  amesema kuwa  atawaondoa watu wote wanaokwamisha wawekezaji na utoaji wa mizigo bandarini kabla hajatolewa yeye na hivi sasa ameanza kazi ya kuchuka majina ya watu wote walio chini yake ili kuanza kuwafatilia.

 Alisema Tanzania na China zimekuwa na ushirikiano wa muda mrefu na serikali ya Tanzania itaendelea kuwaunga mkono wawekezaji wenye nia njema kwa serikali hasa katika kipindi hiki cha kuelekea uchumi wa viwanda.




Aliwapongeza pia watu wote wenye nia ya kuwekeza hapa nchini katika miradi mbalimbali ya viwanda kwa upande wa mazao kama vile muhogo, zao ambalo sasa ni muhimu na lenye kuweza hata kuuzika nje ya nchi.
 


Naye Balozi mpya  wa China hapa nchini, Bi Wang Ke, amempongeza Mwenyekiti wa kampuni hiyo ya CNBM, Song Zhiping, kwa kuanzisha kituo hicho ambacho kitakuwa muhimu na kitatoa fursa fursa kwa wakazi wa maeneo hayo katika kupata ajira.  .

No comments

Powered by Blogger.