JUKATA KUOMBA MAANDAMANO MAHAKAMANI
Jukwaa la katiba nchini (JUKATA) limesema litafungua kesi na kwenda mahakamani kudai haki ya maandamo ambayo wamedai wamenyimwa na jeshi la polisi nchini kwa kile walichopanga kuandamana octoba 30 mwaka huu kwa lengo la kumpongeza raisi magufuli na kudai katiba mpya ambapo wanadai wamepewa sababu nyepesi za kutokuandamana na jeshi hilo
Akizungumza na wandishi wa habari mapema Leo jijini dar es salaam mwenyekiti wa jukwaa hilo Hebron Mwakagenda amesema kuwa
Dunia kote muhimili wa mahakama ndiyo chombo mahususi cha kudai haki pale mtu ama watu wanapoona haki zao zimenyimwa ama zinakandamizwa huku akidai jeshi la polisi limekuwa likiminya haki za kikatiba zinazopatikana kwenye katiba ya Tanzania ibara 18 (a), (b),(d) pamoja na 20 (b))
Aidha amesema kuwa wameshaandaa mawakili wasomi wasiopungua kumi wakiongozwa na Dkt.Rugemeleza Nsha wataongoza mchakato huo wa kudai maandamo ya amani ya kudai Katiba
Post a Comment