|
.
|
Zaidi ya
walimu 100 kutoka Chama cha Walimu Tanzania (CWT) wamejitokeza kupima ugonjwa
wa saratani ya shingo ya kizazi pamoja na kupewa elimu kwa ajili ya kwenda
kuwafundisha wanafunzi ili kuepukana na ugonjwa huo.
Imeelezwa kuwa wakina mama nchini wametakiwa kuwa na mwamko
wa kwenda hospitali kila mwaka kufanyiwa uchunguzi wa Magonjwa ya Saratani
hususani ya Shingo ya Kizazi kwani unapogundulika katika hatua za mapema
unatibika
Akizungumza na waandishi wa Daktari
Bingwa wa Upasuaji wa Magonjwa ya Saratani kutoka Hospitali ya TMJ, Dk.Walter Kweka
wakati wa zoezi la utoaji elimu na upimaji wa ugonjwa huo kwa walimu amesema kuwa
zoezi hilo limaratibiwa na Hospitali ya TMJ kwa kushirikianiana na
Lion Klabu ya Dar es Salaam.
Amesema kuwa unapoona kuna mabadiliko
katika kifua au matiti watu wawe na mwamko kwenda kuchunguzwa ili kuepuka
ugonjwa huo.
Akizungumzia kuhusu elimu wanayo toa kwa walimu hao, Dk. Kweka amesema elimu
hiyo itawaongezea ufahamu katika masuala ya saratani, ikiwemo ya shingo ya
kizazi pamoja na saratani ya matiti na saratani nyingine.
Amesema lengo wanapojua waweze
kujisaidia pamoja na kusaidia katika kuibua wagonjwa ambao wanakuwa na dalili
za ugonjwa huo mapema katika jamii ili waweze kufika sehemu sahihi kwa ajili ya
kufanya uchunguzi mapema kwani unapogundulika ukiwa kwenye hatua za awali
unatibika.
Ameongeza kuwa wamechoka
kupokea wagonjwa ambao wemekwishachelewa na mwisho wa siku mzigo kuwa kwa
hospitali na madaktari kwa kushindwa kumsaidia.
Kwa upende wake Gavana wa Lion
Klabu kwa nchi za Tanzania, Uganda na Sudani Kusini Rizwan Qudri, amesema zoezi
hilo linafanyika bure na ni zuri kwa ajili ya walimu hao kuangalia afya zao
dhidi ya ugonjwa wa saratani ya shingo ya kizazi.
Amesema katika upimaji wa leo lengo ni kupima walimu 100 na kuele kuwa
wanatarajia pia kufanya zoezi hilo katika maeneo mengine nchini.
Amewataka watu wawe wanajitokeza kwa wingi inapotokea fursa kama
hiyo ili waweze kuchunguza afya zao.
Post a Comment