ALICHOKISEMA WAZIRI MPINA KUHUSU MIFUGO INAYOUZWA HOVYO HOVYO
Waziri
wa Mifugo na Uvuvi Mh.Luhaga Mpina amemepiga marufuku mifugo
inayokamatwa kwenye hifadhi mbalimbali nchini kupigwa mnada bila maafisa
mifugo kuipima na kujiridhisha ili kuepuka kuenea kwa magonjwa ya
wanyama hao sambamba na kuwachukulia hatua kali wananchi ambao wamekuwa
wakipokea na kubeba dhamana ya mifugo kutoka nje ya nchi huku wakidai
kuwa ni ya kwao.
Akishiriki
zoezi la ukamataji wa mifugo zaidi ya mia moja na sabini iliyoingia
wilayani Kasulu mkoani Kigoma kutoka nchi jirani ya Rwanda Waziri Mpina
amesema ni kinyume cha sheria na amewataka wafugaji wanaokamatiwa mifugo
yao kujitokeza mara moja ili kuepuka usumbufu unaojitokeza.
Aidha
Waziri Mpina amesema serikali itaendelea kuwachukulia hatua kali
wananchi ambao wamekuwa wakipokea na kukubali kubeba dhamana ya mifugo
kutoka nje ya nchi huku wakidai kuwa ni ya kwao.
Post a Comment