Header Ads

header ad

MAKONDA AKABIDHI MAGARI 18 YA KISASA KWA JESHI LA POLISI



Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mheshimiwa *PAUL MAKONDA* leo amekabidhi *Magari ya kisasa 18 kati ya 26* yaliyopelekwa Mkoani Kilimanjaro *yakiwa Mabovu* (Mkweche) kwaajili ya kufufuliwa upya.


Magari hayo *yalipelekwa Kilimanjaro yakiwa yamebebwa kutokana na ubovu* lakini  sasa yanarejea Dar es Salaam yakiwa Mazima na *Mwonekano kama Magari ya UN* ambapo yatakuwa na uwezo wa kubeba *Askari 11 wakiwa wamekaa na silaha zao.*

Akikabidhi Magari hayo kwa Jeshi la Polisi leo *RC MAKONDA* amesema yataenda kuhudumia Wananchi kwa *kuimarisha Ulinzi na Usalama jijini Dar es Salaam.*

Amesema kuwa kilichomgusa kuboresha Jeshi la Polisi ni Baada ya kuona *Askari wakifanya kazi katika mazingira magumu na wakati mwingine kuvamiwa na majambazi kisha kuuawa na kuporwa Silaha.*

Aidha *RC MAKONDA* ameishukuru kampuni ya *Rajinder Motors Ltd (RSA)* kwa kumuahidi kutengeneza *Magari 56* ya Polisi Dar es Salaam *bila kutumia fedha za serikali (Bure).*

*MAKONDA* ametumia Makabidhiano hayo kutuma *salamu kwa Majambazi, Vibaka* na wale wenye nia ya kuvuruga Amani na Usalama kuwa *kiama chao kimefika.*

Amesema *alipotangaza mpango wa kufufua Magari yaliyokufa wapo waliombeza lakini sasa wanajionea Magari yakiwa Mapya.*

Makabidhiano hayo yameshuhudiwa pia na *Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro ANNA MGWIRA, Kamanda wa Polisi kanda Maalumu ya Dar ea Salaam Lazaro Mambosas* na viongozi wengine wa vyombo vya Ulinzi na Usalama ambapo wamempongeza *RC MAKONDA* kwa ubunifu mkubwa alionao.
 


No comments

Powered by Blogger.