Chama cha Wananchi(CUF), upande wa Profesa Ibrahim Lipumba kimesema kitashiriki kikamilifu katika uchaguzi wa madiwani uliopangwa kufanyika Novemba 26 lakini kimesisitiza kutoshirikiana na Ukawa. Hii ni mara ya kwanza kwa chama hicho kuweka msimamo wake katika uchaguzi tangu kumalizika kwa Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 ambapo CUF ilikuwa miongoni mwa vyama viliunda umoja huo kwa kuweka wagombea waliokubaliana. Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa CUF, Abdul Kambaya amesema leo Jumamosi jijini kuwa chama hicho hakioni sababu yoyote ya kushirikiana na vyama vingine kwenye uchaguzi huo ambao unahusisha halmashauri 34.
Post a Comment