TANI 55,000 ZA MBOLEA ZAINGIA NCHINI
Wafanyakazi wa Mamlaka ya Bandari nchini wakiendelea na zoezi la upakiaji wa mbolea ya kupandia tani elfu 23 tayari kwenda kwa wakulima mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
Wafanyakazi wa Mamlaka ya Bandari nchini wakiendelea na zoezi la kufunga mbolea ya kupandia katika mifuko tayari kwa kupakiwa na kusafirishwa kwenda kwa wakulima.
Kaimu Mkurugenzi Mamlaka ya Udhibiti wa Ubora wa Mbolea Tanzania(TFRA) Bw. Lazaro Kitandu (katikati) akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari wakati zoezi la upakuaji wa mbolea ya kupandia ukiendelea katika bandari ya Dar es Salaam mapema hii leo.
Jumla ya tani elfu hamsini na tano(55,000/=) za mbolea zimeingizwa hapa nchini ikiwa ni hatua ya Serikali ya kuwapatia wakulima mbolea yenye bei nafuu ili kuwasaidia kuzalisha mazao ya kutosha na kuendana na sera ya Tanzania ya Viwanda.
Hayo yamesemwa na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Udhibiti MboleaBw.Lazaro Kitandu wakati akizungumza na wanahabari katika bandari ya Dar es salaam wakati wa zoezi la upakuaji wa mbolea hiyo.
Bw.Kitandu amesema kuwa tani elfu thelathini na mbili za mbolea ya kukuzia ( UREA) imeagizwa kutoka nchini Urusi, huku mbolea ya kupandia ikiwa tani elfu ishirini na tatu aina ya (DAP)imeagizwa kutoka Nchini Morocco ambapo mbolea hiyo itatumika hadi mwezi Desemba mwaka huu.
Aidha amesema kuwa mbolea hiyo siyo ya ruzuku bali ni mbolea iliyodhibitiwa kutoka katika chanzo na kwamba itauzwa kulingana na bei elekezi kutoka serikalini huku akiwaonya wafanyabishara ambao watauza kinyume cha bei elekezi kuwa watachukuliwa hatua za kisheria..
Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mtendaji wa mamalaka hiyoBw.Lazaro Kitandu kwa amesema kuwa msimu huu wa kilimo mahitaji ya mbolea kwa Taifa ni tani laki nne(400000/=)hadi laki nne na nusu(450000/=),huku akisissitiza kuwa endapo viwanda vya kutengeneza mbolea vilivyopo hapa nchini vitaweza kutengeneza mbolea ya kutosha itasidia kupunguza gharama kubwa ya kuagiza mbolea kutoka nje ya nchi.
Post a Comment