Header Ads

header ad

TGNP YABAINI MAPUNGUFU KATIKA KUKUZA NA KUENDELEZA USAWA WA KIJINSIA


Mwenyekiti wa Bodi ya TGNP Mtandao, Mwenyekiti wa Bodi ya TGNP, Vicensia Shule (katikati) alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuelezea yaliyojiri katika siku nne za Tamasha la Jinsia Tanzania Mwaka 2017. Wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP Mtandao, Bi. Lilian Liundi pamoja na wanaharakati mbalimbali walioshiriki tamasha hilo
Sehemu ya wageni waalikwa kwenye Tamasha la Jinsia Tanzania 2017 lililofanyika ndani ya viwanja vya TGNP Mabibo jijini Dar es Salaam wakifuatilia mada mbalimba
Tamasha la Jinsia 2017 lililoandaliwa na TGNP Mtandao kwa kushirikiana na wadau mbalimbali lililofanyika kwa siku nne jijinia Dar es Salaam, limebaini bado kuna changamoto ya utengwaji wa rasilimali katika kukuza na kuendeleza usawa wa kijinsia na kuwawezesha wanawake.

Tamasha hilo pia limebaini mapungufu katika mfumo wa kukusanya takwimu, hasa za umiliki wa ardhi, hivyo kushauri zoezi zima kufanyika kwa umakini ili kuonesha mgawanyo wa umiliki wa ardhi wa wanawake, ukatili wa kijinsia na mimba za utotoni.
Kauli hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa Bodi ya TGNP Mtandao, Mwenyekiti wa Bodi ya TGNP, Vicensia Shule alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuelezea yaliyojiri katika siku nne za Tamasha la Jinsia Tanzania Mwaka 2017.
Aliwaambia waandishi wa habari kuwa masuala mengine yaliyoibuliwa na washiriki ni pamoja na kushauri uwekezaji katika sekta ya kilimo uende sambamba na hali halisi ya uzalishaji ili kuboresha maisha ya wananchi na kuchangia ipasavyo katika Tanzania ya viwanda.
Aidha wameshauri sera mbalimbali za kumwezesha mwanamke na kuinua usawa wa kijinsia uendane na mazingira ya sasa, huku wakitaka bajeti kuu na bajeti za serikali za mitaa zizigatie mahitaji ya kijinsia kwa makundi yote.
“…Tanzania ya viwanda na kuelekea uchumi wa kati inahitaji nguvu kazi yenye afya bora na weledi. Hivyo basi mikakati ya kupunguza vifo vya akinamama na watoto ni muhimu. Hivi sasa watoto 67 kati ya vizazi hai 1000 na wanawake 556 kati ya 100,000 wanakufa kutokana na huduma duni za afya ya uzazi,” alisema Mwenyekiti huyo wa Bodi ya TGNP, Bi. Shule.
Pamoja na hayo, washiriki wameibuwa changamoto ya upatikanaji wa maji safi na salama ambayo imekuwa ikiwakandamiza akinamama kwani wengi bado wanatembea kati ya saa tatu hadi tano kutafuta maji, hali ambayo wameshauri iangaliwe kwa mapana kumpunguzia mzigo mwanamke.
Tamasha la jinsia la 14 lililomalizika Septemba 8, 2017 limemalizika baada ya siku nne za sharehe, tafakuri, mijadala na kutolewa pongezi kwa waliofanya vizuri katika nyanja mbalimblia.

No comments

Powered by Blogger.