LHRC WALAANI VITENDO VYA UKIUKAJI WA SHERIA
Wadau na mashirika ya utetezi wa haki za binadamu Tanzania wamelaani shambulio na jaribio la kuuwawa kwa Mh.TUNDU LISSU ambaye ni mbunge na ni Raisi wa chama cha wanasheria Tanganyika (TLS) lililofanyika mkoani Dodoma.
P
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Dk.HELEN KIJO-BISIMBA amesema wao kama watetezi wa haki za binadamu wamekuwa wakifuatilia kwa ukaribu matukio mbalimbali ya kikatili na yasiyokubalika yanayoendelea nchini kinyume na haki za binadamu .
Aidha Dk BISIMBA amesema matukio haya yanaota mizizi kwa kukosa ufumbuzi na hivyo kuongeza hofu baina ya wapenda amani ,watetezi wa haki za binadamu pamoja na wananchi kwa ujumla.
Dk.BISIMBA ameongeza kuwa Mh.TUNDU LISSU baada ya kuchaguliwa kuwa mbunge na wananchi Singida Mashariki ameendelea kuwa mtetezi wa utawara bora,haki za kisiasa,misingi ya haki za binadamu na rasilimali za Taifa.Hivyo jitihada zake pamoja na wadau wengine zimeweza kuleta matokeo makubwa ikiwemo hatua mbalimbali ambazo Serikali ya awamu ya Tano imezichukua ikiwa pamoja na kubadilisha sheria za madini na petroli pamoja na kuanzisha majadiliano na makampuni ya madini.

Post a Comment